• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

DC Magessa Afanya Ziara ya Kushtukiza

Imetumwa : March 28th, 2018

Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe Tumaini Magessa akikagua Kitabu cha mahudhurio ya watumishi wa hospitali ya wilaya ya Kiteto wakati wa ziara yake hospitalini hapo mchana wa leo.


.....HABARI KAMILI......


Mkuu wa wilaya ya Kiteto mheshimiwa  Tumaini Magessa  amefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya wilaya ya Kiteto, ambapo  amekagua idara ya wagonjwa wa nje(OPD), wodi ya wanaume, wodi ya wanawake ,wodi ya watoto,wodi ya wazazi, kliniki ya magonjwa sugu yasiyo ambukiza (sukari, shinikizo la damu na magonjwa ya akili) ,kitengo cha matibabu ya wagonjwa wa bima ya afya (NHIF) pamoja na kitengo cha dawa na vifaa vya tiba.Ziara hiyo imefanyia leo tarehe 28/03/2018 majira ya mchana.

Akiwa katika idara ya wagonjwa wa  nje, Mhe. Magessa amekagua kitabu cha mahudhurio ya watumishi wa hospitali hiyo ,ambapo amebaini  kuwa watumishi 16  wamechelewa kuingia kazini .Kufuatia uchelewaji huo Mhe. Magessa amesema “ Watumishi 16 wamechelewa kufika kazini leo . Hapa mnahusika na maisha ya watu,lazima umakini uwepo. Msimamizi wa hospitali nitafuatilia kujua ni hatua gani mmewachukulia watumishi hawa. Nataka kuona watumishi  hawa wakichukuliwa hatua.Watumishi wawahi kazini, na sio kuwahi tu, wawepo kwenye maeneo yao ya kazi, na wafanye kazi ’’.

Kadhalika katika kitengo cha matibabu ya wagonjwa wa bima ya afya Mhe. Magessa  amewataka watumishi wa kitengo hicho kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa ili kupunguza malalamiko ambayo yamekuwa mengi kutoka kwa wagonjwa wanaopata huduma za matibabu kwa kutumia bima.Mhe. Magessa amesema ‘‘Ninyi mnafanya kazi ya uuguzi, katika kazi hii mnahudumia watu ambao wanakuja hapa wakiwa na matatizo makubwa kuliko mnavyofikiria.Kauli zenu zinatakiwa ziwe nzuri, kauli zinapokuwa mbaya, wagonjwa wanapokuja hapa wanaongeza shida zaidi ya zile walizokuja nazo’’.


Katika kitengo cha dawa na vifaa vya tiba , Mfamasia wa wilaya ya Kiteto  Mfamasia Mohamed Temba amemueleza Mkuu wa wilaya changamoto kubwa inayowakabili katika kitengo hicho,ambayo ni  MSD kutokuwa na baadhi ya dawa  na vifaa vya tiba , ambapo wamekuwa wakiagiza dawa na vifaa vya tiba hivyo mara kadhaa lakini hawaletewi. Kufuatia changamoto hiyo ,Mhe. Magessa amewataka watumishi wa kitengo hicho kuandaa orodha ya dawa  na vifaa vya tiba vyote ambavyo upatikanaji wake MSD umekuwa ni changamoto ili aweze kulitafutia ufumbuzi suala hilo katika ngazi zinazohusika.


Aidha Mhe. Magessa  amewataka madaktari walioko katika kliniki ya magonjwa sugu yasiyo ambukiza ( sukari , shinikizo la damu na magonjwa ya akili) kuelekeza nguvu katika kuelimisha zaidi  juu ya namna ya kuishi  ili kuepuka magonjwa hayo ,badala ya  kushughulika na  wagonjwa  pekee ,kwani kufanya hivyo hakuwezi kupunguza  ukubwa wa tatizo,lakini wananchi wakielimishwa   idadi ya wagonjwa kwa siku za usoni itapungua.

Katika ziara  hiyo Mhe. Magessa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama . Hata hivyo ziara hiyo sio ya kwanza kwa  Mhe. Magessa, kwani amekuwa akifanya hivyo mara kadhaa katika maeneo mbalimbali wilayani Kiteto.


......MWISHO.......




Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa