Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndg. Ismail Ali Ussi, amekabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya TZS 2,800,000 kwa Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la Jinsia ili kusaidia kitengo hicho kufanya kazi kwa ufanisi.
Fedha hizo ambazo ni sehemu ya michango ya Mwenge wa Uhuru, zimelengwa kununua pikipiki ili kuweza kukisaidia kitengo hicho kuendelea na mapambano dhidi ukatili na unyanyasaji wa kijinsia wilayani hapa.
Kabla ya kukabidhi hundi hiyo, Ndg. Ussi alipokea taarifa ya mapambanao hayo wilayani hapa. Moja ya changamoto zilizotajwa kwenye taarifa hiyo ni baadhi ya wahanga kutowataja watuhumiwa hususani kesi za kumpa mimba mwanafunzi licha ya elimu kubwa kutolewa kwa jamii.
Ndg. Ussi amekipongeza kitengo kwa juhudi wanazozifanya na kusema kwamba ni imani yake wataendelea kupambana na ukatili kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa