Shule tano za sekondari Wilayani Kiteto zimepongezwa kwa kufaulisha kwa 100% katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne (CSEE) uliofanyika Novemba 2024.
Pongezi hizo zimetolewa Februari 12, 2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kiteto, CPA. Hawa Abdul Hassan pamoja na Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari, Mwl. Ally Kichuri kwenye Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Upimaji wa Kidato cha Pili (FTNA) na Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne ambayo ilifanyika Novemba 2024.
Shule hizo ni Matui, Sunya, Orkine, Partimbo na Mtetemela. Sambamba na hilo, viongozi hao wametoa pia pongezi kwa Shule za Ndedo, Bwakalo, Partimbo, Orkine na Matui kwa kuongeza ufaulu kwa miaka mitatu mfululizo huku sekondari ya Dongo imepongezwa kwa kuwa shule pekee iliyokidhi ufaulu kwa kigezo cha KPI mtihani wa CSEE.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kupitia Divisheni ya Elimu Sekondari imewapongeza pia wasimamizi wa Elimu wakiwemo Uthibiti Ubora wa Shule, TSC, Maafisa Elimu Kata wote na Wakuu wa shule kwa ushirikiano mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku hususani usimamizi wa mtaala.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa