Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Mhandisi Tmaini Magessa (aliyesimama) Akifungua Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Kiteto
Jana Tarehe 27.11.2019
Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Kiteto Bw. S. Pashua, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Mh. Mohamed Kiondo ya Kiteto na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bi. Beatrice Rumbeli na Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mh. Emmanuel Papian
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bi. Beatrice Rumbeli Akimkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Mhandisi Tumaini Magessa Katika Kikao Hicho.
Toka Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Mhandisi Tumaini Magessa Akifafanua Jambo Katika Katika Kikao Hicho.
Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mh. Emmanuel Papian Akifafanua Jambo Katika Kikao Hicho
Kwa niaba ya Afisa Mipango wa Wilaya ya Kiteto, Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Elishiria Mnzava Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Taarifa ya Idara Katika Kikao Hicho.
Kwa niaba ya Afisa Ardhi Maliasili na Mazingira wa Wilaya ya Kiteto, Bw. Mgweno Akiwasilisha Taarifa ya Idara Katika Kikao Hicho.
Afisa Kilimo Umwagilia na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Christopher Simwimba Akiwasilisha Taarifa ya Idara Katika Kikao Hicho.
Mratibu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bi. Rufina Haule Akiwasilisha Taarifa ya Idara na Kutoa Ufafanuzi Katika Kikao Hicho.
Kwa niaba ya Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Wilaya ya Kiteto na Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Wilaya ya Kiteto , Bw. Maramoko Akiwasilisha Taarifa ya Idara na Kutoa Ufafanuzi Katika Kikao Hicho.
Mhandisi Magiri wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Kiteto, Akiwasilisha Taarifa ya Ofisi Yake na Kutoa Ufafanuzi Katika Kikao Hicho.
Kwa niaba ya Meneja wa Huduma za Misitu Wilayani Kiteto Mtaalamu Toka Ofisi Husika, Akiwasilisha Taarifa ya Wakala wa Misitu na Kutoa Ufafanuzi Katika Kikao Hicho.
Kwa niaba ya Meneja wa Tanesco Wilayani Kiteto Bw. Leichipya Akiwasilisha Taarifa ya Wakala wa Misitu na Kutoa Ufafanuzi Katika Kikao Hicho.
Afisa wa NIDA wa Wilaya ya Kiteto Bw. Ombeni Mbesele Akiwasilisha Taarifa za NIDA na Kutoa Ufafanuzi Katika Kikao Hicho.
Afisa Mtendaji Kata ya Magungu Bw. Juma Maganga Akifafanua Jambo Katika Kikao Hicho.
Bw. Bakari Sali Sefu Akiuliza Swali Katika Kikao Hicho.
Diwani wa Kata ya Bwagamoyo Mh. Yahya Masumbuko (CCM) Akitoa Ushauri Katika Kikao Hicho.
Bw. Gwacha Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Kiteto Akifafanua Jambo Katika Kikao Hicho.
Bw. Ramadhani Omary Machaku Akiuliza Swali Katika Kikao Hicho.
Afisa Mtendaji Kata ya Partimbo Bw. Halidi Mwinyi Akifafanua Jambo Katika Kikao Hicho.
Mwakilishi wa Wafanyabiashara Kiteto Mzee Kanti Akitoa Ushauri Katika Kikao Hicho.
Afisa Mtendaji Kata ya Matui Bw. Mshana Akifafanua Jambo Katika Kikao Hicho.
Diwani wa Kata ya Kaloleni Mh. Christopher Parmet (CCM) Akitoa Ushauri Katika Kikao Hicho.
Afisa Tarafa wa Tarafa ya Kibaa Bi. Dhulfa Mollel Akifafanua Jambo Katika Kikao Hicho.
Afisa Mtendaji Kata ya Kibaya Bi. Vaileti Mwashibete Akifafanua Jambo Katika Kikao Hicho.
Mkurugenzi wa Ushirika wa Wilaya ya Kiteto Bw. Daudi Joshua Akifafanua Jambo Katika Kikao Hicho.
Kwa niaba ya Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bi. Neema Mbwilo Akifafanua Jambo Katika Kikao Hicho.
Diwani Viti Maalumu Mh. Zamzam (Chadema) Akitoa Ushauri Katika Kikao Hicho.
Picha za Hapo Juu ni Wadau Mbalimbali (Wawakilishi wa vyama vya siasa, Dini wazee mashuhuri, wafanya biashara, Viongozi wa Taasisi mbalimbali) wa Kamati Kama Wanavyoonekana.
-------------------------------- HABARI KAMILI --------------------------------
Hayo yamejiri jana tarehe 27.11.2019 katika kikao cha ushauri cha Wilaya ya Kiteto ambapo mwenyekiti wa kikao hicho alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mh. Mhandisi Tumaini Magessa imefahamika. Wakiongea kwa nyakati tofauti wajumbe ambao ni wawakilishi wa Taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali wamesema msimu wa mwaka huu unaonekana kuwa na dalili njema za kupata mvua ya kutosha kwa mujibu wa Taasisi ya hali ya hewa na wao wanavyoona, hii itapelekea kuwepo kwa mazao mengi yatakayopelekea kipato cha wakulima wadogo na wa kati kuongezeka ikiwa ni pamoja na biashara mtambuka kama vile usafirishaji na kupata ajira mbalimbali za kazi za sekta husika na zinazoshabiiana pia. Suala lingine lililokuwa la msingi ni kutokuwepo kwa masoko ya uhakika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto lakini serikali ilishaliona hilo na kulifanyia kazi kwani upembuzi yakinifu wa miundombinu husika na andiko tayari lilishafanyiwa kazi na sasa liko katika ngazi za juu muda wa kuendelea kutoa fedha za miradi mikakati ukianza basi na sisi tutapata. Mradi mkakati huu ni mradi wa soko la mazao la kimataifa ambalo litajengwa, Kata ya Engusero kitu ambacho likishakamilika wakulima wote watatakiwa kuuza kwa ushirika wa soko hilo, kisha wanunuzi wote wakubwa na wadogo watakuwa wananunua pale kwa bei yenye tija kwa ushirika huo tofauti na ilivyo hivi sasa, ambapo ni maelewano kati ya mnunuzi na mkulima akisaidiwa na madalali ambao siku zote huhitaji posho za ziada maarufu kama "cha juu".
Katika kuhakikisha kilimo hiki kinakuwa cha tija Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Mhandisi Tumaini Magessa amesema "hoja kuu ya msingi ni kujitambua kwa kila mmoja wetu ili afuate sheria, kanuni na taratibu za utekelezaji wa masuala mbalimbali ya kijamii na kiuchumi, kwa kuzingatia makundi mbalimbali kuanzia wafanyakazi wa kilimo wanatakiwa muda wote kuwa shambani kuwasaidia wananchi wanaolima kiholela ili walime kisasa, wakulima nao wajitambue kwa kufuata miongozo iliyopo hakuna sababu ya kuanzisha mgogoro wa ardhi kama unafuata taratibu vivyo hivyo kwa mfugaji kwani tutakuwa tunatumia nguvu nyingi kwenye utatuzi wa migogoro ya ardhi badala ya rasilimali ya muda na fedha tunazozitumia katika migogoro hii kuzitumia katika shuguli za kuleta maendeleo katika jamii zetu na familia zetu".
Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Mhandisi Tumaini Magessa aliendelea kwa kusema "kila mfanyakazi anatakiwa awe na shamba linaloanzia ekari 1 ambayo gharama zake kwa ekari hiyo kwa mwaka ni kati ya Tshs. 160,000/= hadi 180,000/= kwani faida ya kufanya hivi ni kupunguza gharama za maisha badala ya kutumia fedha za mshahara kununua unga basi tumia mazao yako uliyovuna kuandaa chakula cha familia yako, pia ukivuna zaidi ya matumizi yako utaweza kuuza na kuongeza kipato kitakachokuwezesha kufanya mambo mengine ya msingi ya familia yako".
Katika uwasilishwaji wa taarifa mbalimbali za sekta tofauti tofauti wajumbe wamepaza sauti kuwa katika kuongeza mapato ya Halmashauri hususani kwenye vyanzo vipya kama hii ya "wanaomiliki wanyama na mashamba" kuna sheria ndogo ndogo za Halmashauri ya kukusanya ushuru ambazo bado hazijapitishwa ngazi za juu kitu ambacho kinakwamisha upanuaji wa wigo katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri, hivyo tunasisitiza ufuatiliaji uendelee ili zipatikane mapema. Kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano katika kutoa taarifa na msaada wa masuala ya utabiri wa hali ya hewa zinarushwa kwenye Radio Sauti ya Injiri Moshi na pia mwananchi yeyote anaweza kutumia namba zifuatazo 0784 105 787 uki "beep" tu utapigiwa na 0784 105 727 andika ujumbe wa maandishi utajibiwa. Hata hivyo katika kuwasaidia wakulima wafike mbali kimitaji kuna Shirika la mikopo kwa sekta ya kilimo liitwalo "PASS - Private Agricultural Support Sector" ambalo husaidia wakulima katika nyanja za kilimo kimitaji, haya yametolewa na Afisa Ushirika Wilaya ya Kiteto Bw. Joshua Daudi.
Kuhusu Sekta ya Elimu Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Mhandisi Tumaini Magessa amesema "kila Kijiji na Kata kinatakiwa kiwe na mpango endelevu juu ya sekta ya elimu ili kuweza kukabilina na changamoto za madawati, madarasa, mabweni na chakula cha wanafunzi na serikali itasaidia pale wanapoona na wao wanajitambua kuchangia miradi ya maendeleo ya sehemu zao, serikali inaendelea kusaidia ikiwa ni pamoja na kuleta waalimu na kuwalipa mishahara, vitabu na vinginevyo".
Kwenye sekta ya barabara Kiteto ina jumla ya barabara zenye urefu wa kilometa 1291.37 kati ya hizo asilimia 32.18 ni barabara nzuri kabisa, asilimia 25.43 ni za wastani kwa uzuri na asilimia 42.39 ndizo zenye hali mbaya. Lakini kwa mwaka wa fedha huu wanatarajia kupewa fedha kiasi cha Tsh, 1.52 bilioni kwa ajili ya barabara kiasi ambacho kitasaidia kupunguza asilimia ya barabara mbaza zaidi Wilayani Kiteto. Hata hivyo katika barabara hizi nzuri hazikuwa kwa asilimia hii lakini ni baada ya kufanya kazi ya ziada hadi kufikia kiwango hicho ambapo kwa sasa bado Ofisi ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) wanaendelea kuipunguza kwa kadri upatikanaji wa fedha utakavyoruhusu. Kwa ujumla wake Meneja wa Barabara Vijijini na Mjini Mhandisi Magiri amesifiwa sana kwa kusimamia vizuri na sasa barabara ni za viwango yaani upana wa kutosha, ushindiliaji unaostahili na kugusa maeneo mengi ya mji wa kibaya na mitaa yake yote, hivyo basi akiongezewa fedha za kutosha tunaimani kabisa kuwa thamani ya fedha itaonekana zaidi ya ilivyo sasa kwani litafanyiwa kazi eneo kubwa kitu ambacho mwananchi anawekewa mazingira wezeshi na fursa ya kuitumia kiuchumi na pia serikali kutumia fedha kwenye barabara za maeneo mengine.
Hakika yote haya yamefikia katika hatua hii nzuri ambayo kwa sasa ni endelevu ni kwasababu ya uongozi mzuri wa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Mhandisi Tumaini Magessa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Tamim Kambona kwa ushirikiano chanya kati ya wananchi na viongozi wa taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali ndani na nje ya Wilaya ya Kiteto.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa