Shule ya Msingi Olchaniodo imepokea jumla ya shilingi 182,700,000 kutoka serikali kuu kupitia programu ya BOOST, kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya elimu.
Kati ya fedha hizo, shilingi 100,000,000 zitatumika kujenga vyumba vinne (4) vya madarasa ya elimu msingi, huku shilingi 12,600,000 zikielekezwa katika ujenzi wa matundu sita (6) ya vyoo.
Aidha, kiasi cha shilingi 69,100,000 kimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya mfano ya elimu ya awali pamoja na matundu mengine sita (6) ya vyoo, na shilingi 1,000,000 zitatumika kwa shughuli za ufuatiliaji katika ngazi ya shule.
Utekelezaji wa mradi huu unatarajiwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, sambamba na kuongeza fursa ya upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wa eneo hilo.
Tayari wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wameshautambulisha mradi huo kwa serikali ya kijiji ambayo sasa wamepewa jukumu la kwenda kuutambulisha mradi huo kwa wananchi. Zoezi la kuutambulisha mradi kwa serikali ya kijiji limefanyika Julai 21,2025 shuleni hapo.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa