• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi 2017 yafana Wilayani Kiteto ambapo kauli mbiu ni “UCHUMI WA VIWANDA ULENGE WAFANYAKAZI”

Imetumwa : May 1st, 2017

Mgeni Rasmi Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh.Tumaini Magessa akihutubia wafanyakazi na wananchi wa Wilaya ya Kiteto katika kilele cha siku ya wafanyakazi Duniani Mei Mosi iliyofanyika Kiwilaya Kiteto katika Uwanja wa Mpira wa Wilaya Mei 1,2017

Maandamano ya Wafanyakazi wakiongozwa na Jeshi la Polisi na Bendi ya Matarumbeta toka Makao Makuu ya Wilaya kwenda Uwanja wa Mpira 

Wafanyakazi wakipita katika Jukwaa Kuu kwa Mgeni Rasmi 

Wafanyakazi katika Ishara ya Mshikamano daima

Katibu wa CWT - Kiteto (W) Mwl.Rosemary Mwakibete akisalimia Wafanyakazi

Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe hii Bi. Zahra Goda akisoma Risala kwa usaidizi wa Bw. Msechu


Vikundi vya Taasisi mbalimbali katika uimbaji wa Mashairi




Sherehe hii ilijaa Burudani na Michezo mbalimbali ya kufukuza kuku na kuvuta kamba kwa vyama vyote

Mtumishi kutoka Idara ya MIPANGO - Bw. Edgar P. Kavenuke akipokea Cheti cha Mfanyakazi Hodari na fedha taslimu.

Baadhi ya Wafanyakazi Hodari wakipokea Vyeti na Fedha Taslimu zilizoanzia Tshs. 200,000/= hadi 500,000/=

Baadhi ya Wafanyakazi Wastaafu kwa mwaka huu wa fedha wakipokea zawadi za Bati toka vyama vyao


Mwenyekiti wa Halmashauri (W) Kiteto Mh. Lairumbe Mollel akipokea Cheti cha Utambuzi

Mkurugenzi Mtendaji (W) akivishwa taji baada ya kupokea Cheti cha Pongezi kwa kujipambanua zaidi juu ya Kusimamia maendeleo ya Wilaya yake kwa dhati mpaka kuweka kambi Kata ya Kijungu na Sunya, Kutenda Haki na Uwazi.


Wanakikundi akina Mama wa CWT Kiteto katika Ujasiliamali wa kutengeneza nguo mbalimbali, Batiki "Boutique", Mashela kwa wanandoa, Shanga, Heleni, Bangili nk, wapo Community Centre Kibaya Mjini. 

  

Mgeni Rasmi Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Bw. Tumaini Magessa akikagua bidhaa na kupata taarifa fupi toka kwa Mwenyekiti wa Kikundi husika. Mgeni Rasmi aliongozana na Viongozi  wa Chama Tawala (CCM) na Taasisi mbalimbali za Wilayani Kiteto katika ukaguzi huu kama wanavyoonekana hapo juu.

Kimsingi tasnia ya Viwanda ni pana kwa hiyo kuongeza thamani ya vitu, kuzalisha na mbinu wezeshi za kimasoko zitasaidia kuongeza kipato na kutoa ajira kwa anayethubutu na kujituma katika kazi hivyo aliwapongeza sana washiriki wa Kikundi hiki.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi TALGWU Wilaya Bibi. Juliana Mtey akimkaribisha Mgeni Rasmi.


Maadhimisho haya Kitaifa yamefanyika Kanda ya Kaskazini Mashariki Mkoani Kilimanjaro na Kiwilaya yamefanyikia Uwanja wa Mpira wa Wilaya ya Kiteto - Mjini Kibaya.


Akizungumza katika Sherehe hiyo kwa wananchi na wafanyakazi waliohudhuria Mgeni Rasmi ambaye ni Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Bw. Tumaini Magessa amesema katika kuendeleza Uchumi wa Viwanda Wilaya ya Kiteto imetekeleza kwa kutenga ekari ishirini na mbili (22) kwa ajili ya Viwanda kwa sasa.


Mgeni Rasmi katika kuhutubia na kujibu mambo ya msingi yaliyowasilishwa  kwa njia ya Mashairi, Mabango  na Risala kuhusu  uchumi wa viwanda ulenge wafanyakazi, ambapo mwajiri  anatakiwa azingatie Haki, Maslahi na Heshima kwa Mfanyakazi.


Mgeni Rasmi amesema katika  Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto haki inatendeka kwasababu  Mkurugenzi  Mtendaji wa Wilaya Bw. Tamim H. Kambona amepewa Cheti cha Pongezi na Utambuzi katika hili kwa hiyo inadhihirisha haki, usawa na uwazi upo. Aliongeza kuwa kinachoendelea kwa sasa ni kuboresha maslahi ya Wafanyakazi wote ambapo kila mtumishi mwenye matatizo yake yaanzie katika Idara husika.


Katika wafanyakazi kutendewa haki  pia wahakikishe wanatimiza wajibu wao kwa kufanya kazi kwa kufuata sheria, weledi zaidi na kustaarabika kiroho “spiritually civilized”  ambapo mtu hupaswi kufanya jambo baya hata kama huonwi.


Mgeni Rasmi amesema Serikali ya Awamu ya Tano iko makini kwa kuongeza jitihada za usimamizi wa ukusanyaji wa mapato na kuziba mianya ya kutopoteza rasilimali za nchi ambapo hii itapelekea kuwa na uwezo zaidi wa kuboresha maslahi kwa wafanyakazi ikiwemo ya kulipa madeni ya wafanyakazi kwa wakati na kusukuma maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.


Katika kuongeza Mshahara wa wafanyakazi si lazima tarakimu ya mshahara ghafi “Basic Salary” kuongezeka  tu bali punguzo la lipa kadiri unavyozalisha ( pay as you earn - PAYE ) pia  imeongeza  kiwango cha fedha kwa Mtumishi anachochukua na Serikali ndicho ilichokifanya.


Ili kuhakikisha watumishi wanaboreshewa maslahi zaidi Mgeni Rasmi aliagiza yafuatayo:-
•Utaratibu ufuatwe ili watumishi wapandishwe vyeo na kulipwa stahili zao
•Waajiri binafsi wote watenge fedha kwa ajili ya kuwaendeleza wafanyakazi wao.


Kuhusu vyeti Feki Awamu ya Pili inakuja kwa kufuatilia vyeti vya taaluma ni halali kiasi gani kwa kila mtumishi, kwa hiyo ukienda shule tekeleza wajibu wako wa kusoma kwa bidii na kuwasilisha cheti halali kwa Mwajiri wako ili stahili zako zifanyiwe kazi.


Hata hivyo amewaasa Wafanyakazi kutorusha kila kitu kwani nyaraka za Serikali hutolewa kwa idhini maalumu na Mkuu wa Taasisi husika hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Mtandao “Cyber Crime Act 2015” na Sheria ya Habari ya Mwaka 2016.


Mapambano dhidi ya Madawa ya kulevya


Mgeni Rasmi alisema alifuatilia na taarifa zilishatangazwa katika vyombo vya habari pamoja na tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ambapo wahusika wapo jela, kwa hiyo Serikali bado inaendelea katika kupambana na madawa ya kulevya  kwa nguzu zote Wilayani Kiteto kuanzia hatua ya Ulimaji, Uuuzaji, Usafirishaji na Utumiaji, Maafisa Watendaji wa Kata wafuatilie katika maeneo yao.


Mwisho,
Amewapongeza wastaafu, wafanyakazi wote hususani watumishi watatu (3)  waliojipambanua Mganga Mkuu (W), Mwalimu Mkuu Sanka na Mkurugenzi Mtendaji (W) Kiteto.


Tudumishe amani na kuijenga Wilaya yetu, Mungu Awabariki.


Katika kuhakikisha sehemu zote watu wanashiriki kikamilifu jioni kulikuwa na mechi kali zilizowakutanisha uso kwa uso wakongwe wa mpira Kiteto  katika mechi ya kirafiki, fuatana nasi mpenzi msomaji …

 




Mgeni Rasmi ambaye ni Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Bw. Tumaini Magessa akizungumza jambo na wachezaji baada ya kukagua timu hizo.


Mgeni Rasmi Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Bw. Tumaini Magessa akizungumza jambo katika Sherehe za Mei Mosi zilizofanyika usiku kwenye Ukumbi wa Community Centre Mjini Kibaya. Mgeni Rasmi alisisitiza, Wafanyakazi wote kufanya kazi kwa uaminifu na kuonyesha tija.


Mkurugenzi Mtendaji (W) Bw. Tamim Kambona akishukuru jambo ambapo ilifahamika kwamba leo ni siku yake ya kuzaliwa.

Matangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI July 23, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA UTENDAJI WA KIJlJI III August 26, 2021
  • TANGAZO LA KUKODISHA VIBANDA March 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEPTEMBA 2023 September 03, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TABIA MBAYA ZA WATUMUSHI ZINAHARIBU SIFA ZA TAASISI

    May 01, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI KITETO LIMEMPONGEZA RAIS SAMIA.

    May 30, 2025
  • PONGEZI KWA WANANCHI KWA KUTUNZA MAZINGIRA

    April 28, 2025
  • TUUENZI MUUNGANO WETU

    April 27, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa