• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Shirika la OIKOS la Italia Laongeza Nguvu Katika Uwekezaji wa Miradi ya Maji Kwa Miaka 3 Wilayani Kiteto.

Imetumwa : November 12th, 2019

Mhandisi Thadeo Mwangonela wa Shirika la OIKOS EAST AFRICA Akiwasilisha Mada Kwa Wadau wa Maji.

Bw. Tamilwai William wa Shirika la OIKOS EAST AFRICA  Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kiteto Mhandisi Stephano Mbaruku  Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.

Kwa katikati ni Afisa Mipango wa Wilaya ya Kiteto Bi. Beatrice Rumbeli Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.

Kulia ni Kaimu Afisa Usafi na Mazingira Wilaya ya Kiteto Bw. Keveratus Sibanganya Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji, Kushoto ni Afisa Mipango Wilaya ya Kiteto Bi. Beatrice Rumbeli.


Bw. Beatus Temba Akimuwakilisha (Afisa Elimu Msingi Wilaya)  Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.

Aliyesimama ni Mchumi Bw. Edgar Kavenuke Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.

Aliyesimama ni Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii  Bw. Rodrick Kidenya Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.

Aliyesimama ni Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Joseph Zablon Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.

Kulia ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Dr. P. Mbota Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.

Aliyesimama ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Irkiushbour Bw. Haiyo Loltikise Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.


Aliyesimama ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Makame Bw. Shaban Katanga Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.





Hao Hapo Juu ni Picha Mbalimbali za Kikao Hicho.



------------------------------------------   HABARI KAMILI ----------------------------------------------

Hayo yamethibitishwa leo tarehe 11.11.2019 katika kikao cha wadau wa maji kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri wa Wilaya ya Kiteto. Akizungumza katika mafunzo ya uimarishaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira Wilayani Kiteto, Mhandisi Thadeo Mwangonela wa Shirika la OIKOS EAST AFRICA amesema kuna shilingi za kitanzania bilioni 5 zitakazowekezwa kwenye miradi ya maji katika Wilaya mbili Simanjiro na Kiteto kwa muda wa miaka 3 kuanzia mwaka huu wa fedha 2019/2020. Mradi huu utajikita katika sekta nne za kipaumbele yaani Afya, Elimu, biashara na Maji ambapo katika afya, elimu na biashara  ni ujenzi wa vyoo vya kisasa vyenye kutumia maji, wakati huo huo katika jamii ambazo hazina maji basi watawekeza katika hilo ili kuondoa adha ya maji kulingana na mahitaji ya eneo husika. Kwa sasa kabla ya mradi kuanza kunatakiwa kufanyika kwa vikao na mafunzo katika ngazi mbalimbali kuanzia Wilaya hadi Vijijini ili kutoa taarifa hizi na kufanya utafiti wa kimahitaji (need assessment) kwa kila Wilaya.

Meneja wa Wakala wa maji mjini na vijijini (RUWASA) Mhandisi Stephano Mbaruku amesema hadi sasa Wilaya ya Kiteto kwa takwimu za maji Vijijini inajumla ya 38.3% ya upatikanaji wa maji vijijini lakini kwa uwekezaji huu wa sasa tutakuwa na uwezo wa kufikia 80% kwa kipindi cha miaka 3 ijayo kama kutakuwa na ushirikiano mzuri baina ya wananchi, RUWASA na OIKOS.

Kwa mara nyingine tena Meneja wa RUWASA Mhandisi Stephano Mbaruku amekemea sana suala la viongozi wa maeneo husika hususani Maafisa Watendaji wa Vijiji na Maafisa Watendaji wa Kata kutofumbia macho suala la uharibifu wa miundombinu ya miradi ya maji katika maeneo yao, ili kuonekana kwa thamani ya fedha za miradi hiyo kwa wananchi.

Katika kuhakikisha miradi hii inakuwa salama na endelevu viongozi katika ngazi za Kata, Vijiji na Vitongoji watumie mbinu suluhishi zitakazopunguza au kuondoa kabisa dhana potofu ya kuharibu miradi kwa kutumia sheria ndogo ndogo, kukaa na wazee mashuhuri wa maeneo husika na kuweka ulinzi shirikishi wa kijamii ili kulinda miundombinu ya maji katika mradi husika.

Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto iko tayari kushirikiana na RUWASA ili kuleta maendeleo endelevu ya maji kwa wananchi wa Kiteto, hata hivyo wameshukuru Shirika la OIKOS kwa kuisaidia Serikali na jamii ya Kiteto kwa ujumla wake kwenye sekta tajwa hapo juu, chamsingi waendelee kuwa nasi bega kwa bega ili kuhakikisha maendeleo ya uhakika yanapatikana na sisi kama serikali tuko tayari kutumia fedha hizi kwa malengo yaliyokusudiwa tu na si vinginevyo.

Katika kuwepo wa miradi hii wadau wamesema la msingi ni kwamba kabla ya kuanza mradi ni muhimu zoezi husika la upembuzi yakinifu likawa la kutumia muda mfupi wa siku zisizozidi 30 na wataalamu wa Shirika hili la OIKOS wamekubali kuwa itakuwa hivyo.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa