• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

SHULE ZAAGIZWA KULIMA ANGALAU HEKA 10.

Imetumwa : November 28th, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, SSI. Mbaraka Alhaji Batenga, ameagiza kila shule ya sekondari  na msingi wilayani hapo kulima angalau heka kumi  ili kuwapunguzia wazazi gharama ya kuchangia chakula shuleni.  

Hayo ameyaongea katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) wilayani hapo kilichofanyika Novemba 27,2023.

Katika kukabiliana na tatizo la lishe nchini, serikali iliamua wanafunzi wote lazma wale  angalau mlo mmoja shuleni. Kutokana na agizo hilo kila mzazi anawajibika kuchangia chakula shuleni.

Mkuu wa Wilaya amesema endapo kila shule watalima angalau heka kumi, mazao yatakayopatikana yatatumika kama sehemu ya chakula hivyo itawapunguzia  wazazi mzigo wa kuchangia chakula.

“Na ili kilimo kiwe chenye tija, ni lazma kuacha kilimo cha mazoea, ni lazma sasa wafuate kanuni bora za kilimo ikiwemo kulima kwa wakati, kupanda kwa wakati, matumizi ya mbegu bora; matumizi  sahihi ya mbolea na kupalilia kwa wakati” amesema Mh. Batenga.

Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza kwa kusema matumizi ya mbolea si lazma iwe mbolea ya dukani bali hata samadi inaweza kuongeza uzalishaji wa mazao.

Katika hatua nyingine, Kaimu Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo, Ndugu Said Sembade, aliiambia Kamati hiyo kua Kampuni ya Minjingu imeahidi kutoa mbolea tani  2 kwa shule 10 za msingi na shule 10 za sekondari.

“Mashamba katika shule hizo zitakazopokea mbolea, yatatumika kama mashamba madarasa. Lengo la utoaji wa mbolea kwenye shule hizo ni kuongeza uzalishaji na tija ili shule ziweze kukeleza agizo la lishe kwa wanafunzi”, aliongeza Sembade.

Matangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI July 23, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA UTENDAJI WA KIJlJI III August 26, 2021
  • TANGAZO LA KUKODISHA VIBANDA March 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEPTEMBA 2023 September 03, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TABIA MBAYA ZA WATUMUSHI ZINAHARIBU SIFA ZA TAASISI

    May 01, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI KITETO LIMEMPONGEZA RAIS SAMIA.

    May 30, 2025
  • PONGEZI KWA WANANCHI KWA KUTUNZA MAZINGIRA

    April 28, 2025
  • TUUENZI MUUNGANO WETU

    April 27, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa