KIKAO CHA KAMATI YA LISHE WILAYA TAREHE 22/01/2022
Kikao cha ndani cha kamati ya Lishe ya Wilaya kilichoketiwa tarehe 22/01/2022 kilikuwa mahususi kwa ajili ya uwasilishwaji wa taarifa za utekelezaji wa shughuli za lishe kwa kipindi cha robo ya pili (Octoba- Disemba 2021).
Katika kikao hicho kilichokuwa chini ya Mwenyekiti wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Bwana Zabroni Lulandala ajenda zipatazo saba (7) zilijadiliwa na taarifa zipatazo 15 kutoka Idara mbalimbali ambazo ni wajumbe wa kikao hicho ziliwasilishwa kwa ajili ya kuonyesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za lishe zilizofanyika ndani ya Halmashauri.
Katika taarifa hizo mafanikio mbalimbali yalianishwa kwa kila idara iliyowasilisha taarifa yake lakini pia changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa shughuli za lishe na hatua za kuzitatua zilizochukuliwa.
Aidha wakati akifunga kikao hicho Mwenyekiti wa kikao Bwana Zabron Lulandala aliwasihi wajumbe kutoka idara husika kusimamia maadhimio wanayojiweke pamoja na kusimamia sheria wakati wa utekelezaji wa shughuli za lishe na kuongeza ufuatiliji ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.
Afisa lishe wa Halmashauri ya Wilaya Bi. Beatrice Lusanjuka akichangia jambo wakati wa uwasilishaji wa Taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa