Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Remidius Mwema Emmanuel, amewaagiza wakuu wa taasisi wote wilayani hapo ambao hawajaweza kuwatambua wafanyakazi hodari kwa mwaka 2024 kufanya hivyo mara moja.
Maagizo hayo yametolewa katika Ukumbi wa Chama cha Walimu (CWT) Kiteto kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo kiwilaya yameadhimishwa Aprili 29,2024.
Katika Maadhimisho hayo ambayo yalitanguliwa na maandamano ya wafanyakazi mbalimbali, watumishi hodari kutoka idara mbalimbali za halmashauri na kutoka baadhi ya taasisi walipongezwa kwa kupewa vyeti vya pongezi pamoja na fedha taslimu.
Akizungumza baada ya kukabidhi zawadi hizo kwa watumishi hodari, Mh. Mwema alionesha kutofurahishwa na baadhi ya taasisi wilayani hapo kutowatambua wafanyakazi waliofanya vizuri zaidi katika taasisi zao kwa mwaka 2024.
“Nafahamu wote kua ni wafanyakazi wazuri lakini lazma yupo mmoja ambaye amefanya vizuri zaidi. Ni vema kuwatambua watu kama hao na kuwapa motisha kwenye siku maalumu kama hii”, amesema Mh. Mwema.
Mh. Mwema ameongeza kwa kusema kwamba kumtambua mfanyakazi hodari haihitaji gharama kubwa hata kama taasisi haipo vizuri kifedha inaweza kumpa cheti peke yake au barua pasipo kiasi cha fedha.
“Sio lazma apewe fedha, hata cheti tu kinatosha, hata barua tu inatosha na kuleta furaha na kuongeza morali ya kazi. Hivyo nina agiza taasisi zote ambazo hazijatawambua wafanyakazi hodari kufanya hivyo haraka iwezekananvyo na nipewe taarifa ifikapo Mei Mosi: aliongeza Mh. Mwema.
.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa