Katibu Mwenezi CCM Taifa CPA. Amos Makalla amewahimiza wananchi wa Wilaya ya Kiteto kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Wakazi ili waweze kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Rai hiyo ameitoa katika Mkutano wa hadhara ambao umefanyika Septemba 9,2024 katika kata ya Engusero.
CPA. Makalla amesema kwamba kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura sio kigezo cha kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa bali kufanya hivyo kutamuwezesha kushiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025.
"Ili kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa unapaswa ujiandikishe kwenye daftari la wakazi, tunafahamu mna kazi nyingi za shambani ila tenga siku moja tu ili ukajiandikishe kwenye daftari la wakazi kwani kwa kufanya hivyo ndio utaweza kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa ambao utafanyika Novemba 27,2024", amesema CPA. Makalla.
Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa litaendeshwa kwa muda wa siku 10 kuanzia Oktoba 11-20, 2024.
"Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi Jitokeze Kushiriki Uchaguzi".
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa