Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Bw.Fadhili Dedani Akizungumza Kwenye Eneo la Uteketezaji Kijiji cha Partimbo.
Mahindi Yenye Sumukuvu Yakimwagwa na Gari Tayari kwa Uteketezaji
Kaimu Afisa Afya Wilaya Bw. Keveratusi Sibanganya Akitoa Maelezo kwa Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya na Wadau Wengine Walioshiriki Katika Uteketezaji Huu.
Wahudumu wa Afya Wakianza Kazi ya Umwagiliaji wa Mafuta Aina ya Petroli Tayari kwa Uteketezaji.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Bw.Fadhili Dedani Akirusha Mti wa Moto ili Kuteketeza Mahindi hayo.
Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mh. Emmanuel Papian akiongea Eneo la Uteketezaji Baada ya kuwakuta Wataalamu wa Afya Wakiwa Eneo Husika Akiwa Katika Safari Zake.
------------------------------ HABARI KAMILI ------------------------------
Katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama kiafya siku zote Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kupitia Idara ya Afya na Mazingira, Mwezi Julai 2019 sampuli za mahindi haya yalichukuliwa kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara na majibu yamepatikana mwezi Septemba 2019 yakionyesha kwamba haya mahindi yanakiwango kikubwa sana cha Sumukuvu. Gunia 38 ni za mfanyabiashara wa Kibaya aitwae Musa Mwamba na zingine gunia 8 zilitokea Kijiji cha Nalang'tomoni ndipo taratibu za kuteketeza mzigo huu zilifuata ikiwa ni pamoja na wahusika kujaza "Surrender Form" inayoonyesha kuridhia kuteketezwa kwa mahindi haya.
Kaimu Afisa Afya wa Wilaya ya Kiteto Bw. Kevaratusi Sibanganya alisema tunafanya hivi kutokana na kanuni na taratibu za kisheria ili kuwaweka salama wananchi wote kwani zaidi ya watotot 9 wamefariki mwezi Julai 2019 katika Wilaya yetu ya Kiteto kutokana na Sumukuvu. Hadi sasa Hospitali yetu ya Wilaya haina vipimo vya kupima sumukuvu ila kitaalamu dalili za mtu kuwa na sumukuvu tunazitambua kwa binadamu yeyote kisha tunawapa rufaa ya kwenda Hospitari ya Benjamini Mkapa Dodoma. Hata hivyo wataalamu wa Shirika la Viwango nchini (TBS) Kanda ya Kaskazini tuliendelea kushirikiana nao katika ufuatiliaji zaidi wa mahindi mbalimbali ambayo yapo stoo na kaya 4 jirani toka Kijiji cha Ndirigishi kwa uchunguzi unaendelea ili kupata majibu na kuweza kuchukua hatua zaidi.Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Bw.Fadhili Dedani alisema elimu ya Sumukuvu ni endelevu lakini hadi sasa wataalamu wa Hospitali ya Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati wameshapewa Elimu hii na namna ya kutambua mgonjwa wa Sumukuvu kwa dalili za awali za kiafya kwa binadamu. hata hivyo Serikali imefanya jitihada kubwa sana za kutoa Elimu hii kwa wananchi kupitia Mikutano mbalimbali ya hadhara katika Vijiji na Vitongoji mbapo vipeperushi vinavyohusiana na Sumukuvu vilisambazwa Wilaya nzima kupitia maeneo yote ya kutolea huduma za afya Wilayani Kiteto ili kufikisha ujumbe wa matumizi bora ya kilimo kuanzia ukuzaji wa mimea, wakati wa mavuno, uhifadhi wa mazao husika na wajibu wa mwananchi na Serikali katika kuhakikisha tunajikinga na kutokomeza ugonjwa huu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, maelekezo yako wazi kwa kila mtu na wanajua kuwa mazao yakiwa na hali fulani ni dalili za sumukuvu kwa hiyo achukue jukumu mwenyewe la kuyateketeza mazao husika haraka au toeni taarifa ofisi ya karibu ya Serikali, isipokuwa kuna wananchi wanaokaidi maagizo haya, lakini yeyote atakayeenda kinyume na maagizo haya ya Serikali atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Mbunge wa Wilaya ya KitetoTunashukuru Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kupitia Idara ya Afya na Mazingira kutekeleza haya kwa vitendo, lakini Wizara ya Kilimo wanalifahamu hili na ndiyo maana wametilia mkazo sana katika ufuatiliaji wa jambo lolote linalohusiana na sumukuvu katika Wilaya yetu.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa