Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh.A.Mnyeti Akihutubia Mkutano wa Hadhara Mjini Kibaya Wilayani Kiteto Alipokuwa Akikamilisha Ziara ya Siku Tano.
Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mh. Emmnuel Papian Akisalimia Wananchi Katika Mkutano wa Hadhara Mjini Kibaya.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Mhandisi Tumaini Magessa Akikaribisha Maswali na Kero Mbalimbali Kwa Wananchi Kujitokeza ili Ziweze Kupatiwa Majibu Katika Mkutano huo wa Hadhara.
Wananchi Wakiuliza Maswali na Kero Mbalimbali Katika Mkutano huo wa Hadhara.
Toka Kushoto Mwenye Njano ni Bi. Suma Afisa wa Mkoa wa Manyara anayeshugulikia Ardhi akiwa na Afisa Ardhi na Maliasili Wilaya Bw. Gurisha Damas Wakisikiliza Maelekezo ya Mh. Mkuu wa Mkoa Katika Mkutano huo wa Hadhara.
Mkaguzi wa Ndani Wilaya ya Kiteto Bw. E. Mnzava Akitoa Ufafanuzi kwa Wazee Hawa.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kiteto Bw. R. Kidenya Akitoa Ufafanuzi wa Maswali na Kero Mbalimbali Katika Mkutano huo wa Hadhara.
Mnganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto Dr. P.Mbota Akitoa Ufafanuzi wa Maswali na Kero Mbalimbali Katika Mkutano huo wa Hadhara.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kibaya Bi. Vaileti Mwashibete Akisoma Taarifa ya Mradi wa Maji hapo Hospitali ya Wilaya Kibaya
Meneja wa TARURA Bw.Magiri Akisoma Taarifa ya Mradi wa Barabara za Mjini Kibaya.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Mnyeti Akitoa Maelekezo.
----------------------------------- HABARI KAMILI -----------------------------------
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Alexander Mnyeti amesema Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhandisi Tumaini Magessa anaongoza kwa utendaji mzuri na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Bw.Tamim Kambona ndiye Mkurugenzi anayeongoza Mkoa wa Manyara kwa uchapakazi ikiwemo kusimamia kwa umakini miradi ya maendeleo inayopelekea wananchi kupunguziwa kero mbalimbali za kupata huduma za kijamii hususani afya, maji na elimu.
Mh.Mkuu wa Mkoa, A.Mnyeti aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi mjini Kibaya alipokuwa anamalizia ziara yake iliyochukua siku tano kuanzia tarehe 12.10.2019 hadi tarehe 16.10.2019 katika kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo miradi ya afya, maji, barabara, elimu na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi Wilayani Kiteto. Wananchi mbalimbali waliuliza maswali kwa Mh. Mkuu wa Mkoa ambapo mengi yalipata ufumbuzi hapo hapo na mengine alitoa maagizo kwa viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Kiteto kuyafanyia kazi kwa vipindi tofauti tofauti na kupewa taarifa ya utekelezaji huo.
Alisema Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mh. Mhandisi Magessa ni mchapakazi mzuri na wa kuigwa katika Mkoa huu wa Manyara kwa kushirikiana na Mkurugenzi wake Bw. Tamim Kambonahivyo viongozi na wananchi kwa ujumla muwape ushirikiano wa kutosha ili Kiteto isonge mbele daima kwani ndiyo dhamira ya Serikali ya awamu ya Tano.
Alisema japokuwa baadhi ya watu wanamlalamikia Mh. Mkuu wa Wilaya huyu lakini maeneo mengine wanatamani kuwa na Mkuu wa wilaya kama Mh. Mhandisi Magessa kwasababu vitu anavyofanya vipo na vinaonekana kwanza anatii na kutekeleza maagizo yote yanayotolewa ngazi ya juu, kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua ambapo kila kata na kijiji nilipofika nikiangalia kitabu cha wageni tayari ameshafika hapo mara kadhaa na Mkurugenzi wake Bw. Kambona.
kwa ujumla wananchi wengi Wilayani Kiteto wamesifu uongozi wa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Mhandisi Tumaini Magessa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Tamim Kambona kwa kutekeleza kwa vitendo utatuaji wa kero mbalimbali za wananchi, kwa mtazamo huu wananchi wanatumia muda mfupi
kupata huduma bora na utumia muda mwingi katika fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii ili kujipatia kipato cha familia zao.
Mh. Mkuu wa Mkoa alisema Pamoja na changamoto zilizopo hapa Kiteto ningekuwa natoa maksi ningewapa 95% kati ya 100% na hii ni kutokana na utendaji mzuri wa uongozi mzima wa Kiteto wakiongozwa na Mh. Mhandisi Magessa na Bw. Tamim Kambona. Mkuu wa Mkoa Mh.Mnyeti alisema nawahakikishieni kuwa Halmashauri inayofanya vizuri kwenye mambo mengi katika Mkoa wa Manyara ni Kiteto.
Alisema utofauti wao na viongozi wa Wilaya zingine za Mkoa huu ni kwamba hapa kuna usimamizi wenye tija wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo sehemu kuu tatu zinajidhihirisha zenyewe ambazo ni ushirikishwaji mzuri wa kamati za ujenzi za miradi husika katika Vijiji na Kata, gharama ndogo lakini majengo mengi (value for money), miradi yote imetumia vifaa vya ujenzi vyenye ubora na wa kupendeza kweli kweli kama vile "gypsum board", uwekaji wa umeme na vingine vingi hivyo wanapaswa kupongezwa.
Alisema viongozi wengine wa Wilaya na Halmashauri za Mkoa wa wangu wa Manyara wanapaswa kuja hapa Kiteto ili wajifunze namna ya kusimamia miradi yao ya maendeleo. Mh. Mnyeti alisema nimezindua na kuweka mawe ya msingi miradi mbalimbali katika Wilaya hii kwani miradi ni bora na yenye kiwango cha juu siwezi kuacha kuizindua kama baadhi ya maeneo ambapo nimepita na kugundua fedha iliyotumika siyo sahihi. Kwanini mmoja katika mkoa huu huu ajenge darasa la ukubwa huo huo kwa milioni 20 na mwingine ajenge kwa milioni 13? alihoji; aliendelea na kusema utofauti wa gharama ni lazima utofautiane lakini si kwa kiwango kikubwa namna hii.
Alisema amefika Kiteto ameshuhudia ujenzi wa baadhi ya miradi ya maendeleo ikiwemo madarasa ambapo fedha za ujenzi wa madarasa matatu lakini wao kwa fedha hizo hizo wamejenga madarasa manne yenye umeme na kiwango kinachokubalika.
Hata hivo Mkuu wa wilaya ya Kiteto, Mh. Mhandisi Tumaini Magessa alishukuru kwa pongezi hizo na kuahidi kuongeza kasi zaidi katika kusimamia utekelezaji wa maagizo mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo, kutatua migogoro ya ardhi na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi vijijini na kuzitatua kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa