Timu ya Madakatari Bingwa na Bobezi wameshawasili Wilayani Kiteto na kuanza kazi ya kutoa huduma kwa wananchi.
Akiongea wakati wakitambulishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mwenyekiti wa jopo hilo la Madakati Bingwa na Bobezi, Dkt. Victor Adolph, amesema kwamba ujio wao ni juhudi za kampeni ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwasogezea karibu wananchi huduma za kibingwa na bobezi.
Aidha, Dkt. Adolph ameongeza kwa kusema kwamba ujio wao pia mbali na kutoa huduma kwa wananchi, unalenga kubadilishana uzoefu na madaktari na wahudumu wa Afya wa Kiteto.
Nae Mkuu wa Wilaya Kiteto, Mh. Remidius Mwema, amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea wananchi wa Kiteto huduma za kibingwa na bobezi maana inawapunguzia wananchi adha ya kusafiri kwenda nje ya Wilaya na Mkoa kwaajili ya huduma hizo.
"Tunamshukuru Mhe. Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujio wa madaktari hawa na tumefurahi maana wapo wananchi wanaohitaji huduma za kibingwa ila kwenda Dodoma ni mbali na unakuta uchumi sio mzuri hivyo mtu anashindwa", amesema Mhe. Mwema.
Nae Mkurugenzi Mtendaji (W) Kiteto, CPA. Hawa Abdul Hassan amemshukuru Mhe. Rais kwa ujio huu wa Pili wa madaktari Bingwa na Bobezi na kuwahamasisha wananchi wa Kiteto kujitokeza ili kuweza kupata huduma kutoka kwa madaktari hao bingwa na bobezi kwani mhe. rais amewasogezea huduma hiyo karibu.
Nae Mganga Mkuu (W), Dr. Vicent Gyunda, amesema timu yake ya afya katika Hospitali ya Wilaya imejipanga vyema kushirikiana na madaktari hao ili kuweza kuwahudumia wananchi wote wanatakaoenda kupata huduma hizo za kibingwa.
Madaktari hao wameanza kutoa huduma Septemba 24, 2024 na wataendelea kutoa huduma mpaka siku ya Jumamosi Septemba. 28, 2024.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa