Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara, Ndugu Peter Toima, ameipongeza Kiteto kwa uamuzi walioufanya wa kubadilisha matumizi ya fedha na kujenga majengo matatu katika hospitali ya wilaya badala ya kufanya ukarabati.
Hayo ameyaongea Desemba 3, 2023 katika majumuisho ya ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Manyara wilayani hapo. Toima amesema, maumuzi ya kujenga majengo hayo mapya badala ya kukarabati yaliyopo yalikua ni maamuzi ya hekima, busara na ya kizalendo.
“Kwakweli nawapongeza sana kwa maamuzi hayo kwani yamezingatia uhitaji uliopo na hakika nikiri kwa kusema kwamba kazi kubwa imefanyika”, aliongeza Ndugu Toima.
Awali akitoa taarifa ya mradi huo Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dr. Orestus Sakweli, amesema kwamba Kiteto ilipokea kiasi cha fedha shilingi 900,000,000 kutoka serikali kuu kwaajili ya kukarabati majengo yaliyopo.
“Kutokana na uchakavu wa majengo yaliyopo, Halmashauri ya Wilaya iliamua kutofanya ukarabati badala yake kuanza ujenzi wa majengo muhimu matatu ambayo ni Jengo la upasuaji, jengo la maabara na jengo la mama na mtoto” alisema Dr. Sakweli.
Awali kabla ya kutembelea mradi huo katika Hospitali ya Wilaya, Ndugu Toima pamoja na wajumbe wa kamati hiyo, walitembelea mradi wa Maji Magungu na kuagiza watendaji wilayani hapo kuhakikisha kua wananchi katika kijiji cha Emarti pia wananufaika na mradi huo.
Mradi wa Maji katika kata ya Magungu ambao unatekelezwa na RUWASA, ulianza kutekelezwa Septemba 2022, na umegharimu kiasi cha fedha Bilioni 1.3. Meneja wa Ruwasa Wilayani Kiteto, Mhandisi Stephano, Mbaruku, amesema kwamba mradi huo umekamilika na kwa sasa unahudumia vijiji viwili kati ya vitatu katika kata hiyo ambavyo ni kijiji cha Magungu na kijiji cha Nhati.
Kabla ya mradi huo kuanza, upatikanaji wa maji katika kijiji cha Magungu ulikua ni 30% na upande wa Nhati ulikua 0% ila mradi huo umefanya upatikanaji wa maji katika vijiji hivyo viwili kwa sasa kuwa 100%.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa