Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viwatilifu Tanzania (TPHPA), wametoa mafunzo ya kuwajengea Maafisa Ugani- Kilimo uwezo wa kutabiri mlipuko wa visumbufu vya mimea.
Mafunzo hayo ambayo yamefanyika Februari 7,2024 katika Ofisi za Kilimo Wilayani hapo, yaliendeshwa na wawezeshaji watatu kutoka TPHPA Arusha ambao ni Gladman Mbukoi, Aniceth Chuwa na Hashim Mwemnao.
Mbali na mafunzo hayo, mamlaka hiyo imetoa vifaa vya kuwasaidia maafisa ugani hao katika zoezi la kutabiri visumbufu vya mimea pamoja na vipima mvua. Visumbufu vya mimea vilivyolengwa kwenye mafunzo hayo ni viwavijeshi.
Ingawa Halmashauri ina kata 23, ila mafunzo hayo yametolewa kwa Maafisa Ugani –Kilimo kutoka kwenye kata nne kutokana na ufinyu wa bajeti. TPHPA inategemea kufanya mafunzo hayo kwa kata zote pale watakapopata bajeti ya kutosha.
Kata ambazo zimenufaika na mafunzo hayo na vifaa hivyo ni Bwawani, Dosidosi, Njoro na Olboroti. Kata hizo zimepata nafasi ya kwanza kwasababu zinahistoria ya kuathiriwa zaidi na visumbufu hivyo.
Nae Kaimu Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Ndugu Said Sembade amesema kwamba lengo la mafunzo hayo ni kuweza kugundua uwezekano wa mlipuko wa visumbufu hivyo ili kuweza kuwasaidia wakulima kukabiliana navyo na kuepeuka kupata hasara.
Mbali na utoaji wa elimu , TPHPA pia hutoa sumu ya kuthibiti/kuua visumbufu pasipo gharama yoyote.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa