Mkuu wa Mkoa wa Manyara akisikiliza maelezo kuhusu ujenzi wa jengo Jipya la Halmashauri ya Kiteto
waliosimama pembeni yake ni Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ndugu Tamim Kambona ( kulia)
Mkuu wa Mkoa wa Manyara pamoja na ujumbe alioambatana nao wakikagua jengo Jipya la Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ambalo ujenzi wake unaendelea
Tumieni Wahandisi wa Ndani – RC Mnyeti
Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti ameiagiza halmashauri ya wilaya ya Kiteto kutumia wahandisi ujenzi walioajiriwa na halmashauri hiyo katika kujenga majengo yake ili kupunguza gharama za ujenzi.Mheshimiwa Mnyeti ameyasema hayo alipokuwa akikagua jengo jipya la halmashauri ya wilaya ya Kiteto lililopo katika kata ya Bwagamoyo ambalo ujenzi wake unaendelea.
Akisisitiza kuhusu kutumiwa kwa wahandisi hao mheshimiwa Mnyeti anasema ‘‘mkurugenzi wakati mwingine mnapokuwa na miradi ya ujenzi kama hivi ,tumia wahandisi wako.Serikali imesomesha wataalamu wake,wataalamu hao wanatakiwa watumiwe katika miradi kama huu ili utaalamu walioupata darasani wautumie kwa faida na maendeleo ya serikali yao’’.
Aidha mheshimiwa Mnyeti amesema kwamba mradi huo gharama yake ni shilingi bilioni 4, na hapohapo mkandarasi hana mtaji anategemea pesa hiyo hiyo anayolipwa ndio afanyie kazi,wakati ingetumika force akaunti ,wahandisi wa ndani na mafundi wa kawaida gharama zisingefika hapo, na yawezekana mradi huo ungekwisha kukamilika.Mheshimiwa Mnyeti ametoa mfano wa ujenzi wa majengo ya ofisi yaliyojengwa makao makuu ya mkoa wa Manyara ( Babati) ambayo kwa kutumia force akaunti , wahandisi wa ndani na mafundi wa kawaida yamegharimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 900 hadi kukamilika.
Force akaunti ni njia ya malipo inayotumika katika majiji, manispaa na halmashauri kwa kazi za ziada katika kazi za ujenzi kama mkandarasi na mhandisi hawako tayari kujadiliana kuhusu bei kwa kazi nyingine mpya zitakazoongezeka. Lengo la kutumia force akauti ni ili mkandarasi afanye kazi za ziada kwa gharama ile ile.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa