Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo akitoa maelekezo baada ya kukagua ujenzi wa mabweni na madarasa katika shule ya sekondari Engusero.
wakuu wa idara za halmashauri na wakuu wa taasisi mbalimbali wilayani Kiteto wakisalimiana na waziri wa OR - TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo wakati alipowasili katika shule ya sekondari Engusero katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Sunya, wilayani Kiteto.
Bweni moja wapo kati ya mabweni mawili yaliyojengwa katika shule ya sekondari Engusero, ambayo yamekaguliwa na Mhe. Selemani Jafo wakati wa ziara yake katika shule hiyo iliyopo kata ya Engusero ,wilayani Kiteto.
Darasa moja wapo kati ya madarasa manne yaliyojengwa katika shule ya sekondari Engusero, ambayo yamekaguliwa na Mhe. Selemani Jafo wakati wa ziara yake katika shule hiyo iliyopo kata ya Engusero wilayani Kiteto.
Mhe. Selemani Jaffo akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugezi Mtendaji( W) Kiteto Ndg. Tamim Kambona kuhusu madarasa na mabweni yaliyojengwa katika shule ya sekondari Engusero, wakati wa ziara yake katika shule hiyo iliyopo kata ya Engusero wilayani Kiteto.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Engusero wakimsikiliza waziri wa OR - TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo wakati akizungumza nao katika ziara yake shuleni hapo kukagua ujenzi wa mabweni na madarasa ,katika shule hiyo iliyopo katika kata ya Engusero, wilayani Kiteto.
Waziri wa OR - TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo akitoa maelekezo kuhusu ujenzi wa barabara ya Namelock - Sunya wakati akikagua barabara hiyo , katika ziara yake wilayani Kiteto .
Waziri wa OR - TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo akikagua makaravati katika barabara ya Namelock - Sunya katika ziara yake wilayani Kiteto .
Jengo moja wapo kati ya majengo yanayojengwa katika kituo cha afya Sunya ambayo yamekaguliwa na Waziri wa OR - TAMISEMI Mhe. Suleimani Jaffo wakati wa ziara yake kituoni hapo kukagua ujenzi huo.
Waziri wa OR - TAMISEMI Mhe. Suleimani Jaffo akisikiliza maelezo kutoka kwa mhandisi wa H/W Kiteto Mhandisi Chogo Mang'era kuhusu ujenzi katika kituo cha afya . Katika ziara yake kituoni hapo kukagua ujenzi huo
Waziri wa OR - TAMISEMI Mhe. Suleimani Jaffo akizungumza na wananchi wa kata ya Sunya katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Sunya, wilayani Kiteto.
Wananchi wa kata ya Sunya pamoja na wakuu wa idara za halmashauri na wakuu wa taasisi mbalimbali wilayani Kiteto wakimsikiliza waziri wa OR - TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Sunya, wilayani Kiteto.
…….. HABARI KAMILI………
Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI mheshimiwa Selemani Jaffo amesema kwamba halmashauri zitaendelea kutumia 'force account', kwa sababu mafundi wanao na wamewaajiri wahandisi katika halmashauri, ambapo kazi yao kubwa ni kusimamia kazi za ujenzi. Mheshimiwa Jaffo ameyasema hayo wakati akikagua ujenzi wa madarasa na mabweni katika shule ya sekondari Engusero, iliyopo kata ya Engusero, wilayani Kiteto jana.
Mhe. Jaffo amesema kwamba utaratibu wa wizara yake kwa sasa ni kutumia 'force account',kwani kwa kufanya hivyo fedha za serikali zinaweza kutimiza malengo yaliyokusudiwa,kwa sababu kuwatumia wakandarasi ni gharama kubwa zaidi tofauti na gharama ambazo zinatumika wakati ambapo kazi za ujenzi zinafanywa na mafundi wa kawaida na kusimamiwa na wahandisi walioajiriwa na halmashauri.
Aidha Mhe. Jaffo amepongeza kazi ya ujenzi inayofanyika katika shule hiyo, ambapo amesema ‘‘Naona kazi inakwenda vizuri,kwa macho ya harakaharaka mmezitendea haki zile fedha, kwa sababu naona bweni hili,na mmeniambia kuna bweni lingine na kuna madarasa manne, yote yanajengwa. Na baadae mtajenga vyoo, matundu matano matano kila bweni.Huu ndio utaratibu wa ofisi ninayoongoza mimi sasa. Nataka kila mtu awajibike, na fedha ikija lazima ilindwe”.
Akionyesha kuridhishwa na kazi ya ujenzi iliyofanyika Mheshimiwa Jaffo amesema ‘‘ndio maana siku zote nimekuwa nikitoa maelekezo kwamba lazima tutumie 'force account' ,pesa tuliyoleta milioni 215 mngesema mtumie mkandarasi,maana yake milioni 215 yote mkandarasi angesema anawatengenezea bweni hili moja peke yake.Lakini kwa sababu imetumika 'force account',tunapata jengo hili limekamilika na vitanda vyake, tunapata jengo lingine la bweni na tunapata madarasa manne”.
Vilevile Mhe. Jaffo amekagua barabara ya Namelock - Sunya yenye urefu wa Kilometa 88.I ambayo ujenzi wake unaendelea ,ambapo ameonyesha kutoridhishwa na kiiwango cha ujenzi wa madaraja na makaravati ,hali iliyomsababisha kutoa agizo la kusitishwa kwa ujen
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa