Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Mhe. Lairumbe Mollel akifungua kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kiteto cha kupitisha bajeti ya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Mhe. Lairumbe Mollel akiendesha kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kiteto cha kupitisha bajeti ya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Ndg. Tamim Kambona akiwasilisha bajeti ya halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwa mwaka wa fedha 2018/2019 wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha bajeti hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
Katibu Tawala wilaya ya Kiteto Ndg. Stephano Ndaki akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya katika kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha bajeti ya halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kiteto Ndg. Mohamed Kiondo akizungumza wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha bajeti ya halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
Wahe. madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa bajeti ya halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwa mwaka wa fedha 2018/2019 wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha bajeti hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
Wahe. madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto wakitoa hoja wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha bajeti ya halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
Wataalamu kutoka idara mbalimbali za halmashauri ya wilaya ya Kiteto wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa bajeti ya halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwa mwaka wa fedha 2018/2019 wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha bajeti hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
..................... HABARI KAMILI..................
“Tutahakikisha Miradi Yote Inakamilika kwa Wakati” DED Kiteto.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Tamim Kambona amesema kwamba watafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba miradi yote ya maendeleo ambayo haijakamilika katika mwaka wa fedha 2017/2018 inakamilika katika mwaka 2018/2019.Ndugu Kambona ameyasema hayo katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kiteto cha kupitisha bajeti ya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2018 /2019 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri mwishoni mwa wiki .
Ndugu Kambona amesema kwamba ipo miradi mingi ambayo haijakamilika kutokana na ukosefu wa fedha, lakini kwa mwaka 2018/2019 halmashauri imejipanga kukamilisha miradi hiyo ili iweze kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa. Akizungumza wakati akijibu hoja mbalimbali za waheshimiwa madiwani ndugu Kambona anasema ‘‘naomba niwatoe wasiwasi waheshimiwa madiwani wote kwamba sisi tunaendelea kuvifanyia kazi vitu vyote.Kwa vile ambavyo viko kwenye bajeti na tunaona fedha hazifiki,tunapopata fedha zetu nyingine zozote tunaelekeza huko ili tumalize.Lengo letu ni kuhakikisha kuwa miradi yote inakamilika. Miradi ambayo haijakamilika mimi inaniumiza kichwa kuliko ninyi waheshimiwa.Nataka miradi hii yote tuliyonayo ambayo haijakamilika,yote ikamilike.Na ni lazima ikamilike. Tunajua fedha za miradi za mwaka huu tulionao tunaoumaliza hatujapokea hata senti moja,kati ya zile bilioni 1.2,fedha hizo nazo zikianza kufika tutazielekeza huko na miradi yote tutahakikisha inakamilika kwa wakati”. Ndugu Kambona amesema kwamba mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 umezingatia sheria ya bajeti namba 11 ya mwaka 2015 .Vile vile mpango huo pia umezingatia ushirikishwaji wa jamii kuanzia ngazi ya vijiji na kata.
Aidha ndugu Kambona ameainisha vipaumbele vya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2018/2019,vipaumbele hivyo ni; Kuboresha mapato ya ndani kwa kutumia mfumo wa kielekroniki,kufanya mipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji 41 vilivyosalia,utoaji wa elimu bila malipo,ukamilishaji wa miradi ambayo haikukamilika katika mwaka wa fedha 2017/2018,ajira za watumishi na upandishaji wa vyeo,utawala bora kwa maana ya mikutano ya kisheria ikiwemo ndani yake,stahili za watumishi,kutenga asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa ajili ya maendeleo ya vijana,wanawake na walemavu,kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji kutoka 37% hadi 55% ,kuongeza kiwango cha ufaulu wa kumaliza elimu ya msingi kutoka 60% hadi 80%, kuwezesha uanzishwaji wa viwanda vipya vidogo vidogo na vya kati 15,kusimamia amani na utulivu ili kuweka mazingira mazuri kwa wadau kutekeleza shughuli za maendeleo,pia kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Kadhalika ndugu Kambona ameainisha mafanikio yaliyopatikana katika mwaka wa fedha 2017/2018 ambapo katika sekta ya maji, halmashauri imefanikiwa kuchimba visima saba katika vijiji vya Ndedo, Makame,Kijungu,Ndirgishi Lembapuri,Engongare na Sunya ,kazi ya uchimbaji wa visima hivyo imekamilika, kazi ya kufanya usanifu kwa ajili ya usambazaji wa maji katika vijiji hivyo inaendelea ili maji .Katika sekta ya afya halmashauri imefanikiwa kuongeza upatikanaji wa dawa,vifaa tiba na vitenganishi kutoka 60% hadi 80%. Kuvuka kwa lengo la taifa la asilimia 90% na kufikia 95% katika utoaji wa matone ya vitamin A kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi miaka 5. Kufikia lengo la taifa la 60% katika huduma za uzazi wa mpango .Kwa upande wa elimu msingi imefanikiwa kuboresha miundo mbinu katika baadhi ya shule,utengenezaji wa samani kwenye shule za msingi na sekondari, ujenzi na ukamilishwaji wa vyumba vya madarasa na uboreshaji wa miundombinu. Katika sekta ya ardhi ,vijiji 22 vimeandaliwa mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa lengo la kuondoa migogoro. Mashamba 3014 yamepimwa,ambapo mashamba 1205 yanaandaliwa hati miliki za kimila. Mipaka ya vijiji vyote 63 imepimwa upya na kupangiwa ramani za upimaji kwa kila kijiji.
Katika hatua nyingine ndugu Kambona ameainisha changamoto mbalimbali zinazoikabili halmashauri katika mwaka wa fedha 2017/2018 ikiwemo kuchelewa kwa ruzuku ya miradi ya maendeleo,ambapo amesema kwamba hadi kufikia mwezi Desemba kiasi cha shilingi bilioni 2.6 tu sawa na 34% ya bajeti yote ndizo zilizokuwa zimepokelewa kati ya shilingi bilioni 7.7. Kukosekana kwa mvua za kutosha kumesababisha mapato kushuka, kwa kuwa mapato mengi ya halmashauri hutegemea mazao ya kilimo na mifugo. Sambamba na changamoto ndugu Kambona amebainisha mikakati ya halmashauri yake katika kukabiliana na changamoto hizo katika mwaka wa fedha 2018/2019, mikakati hiyo ni; kuendelea kufuatilia kwa karibu upatikanaji wa ruzuku ya maendeleo kwa kupitia ofisi ya katibu tawala mkoa wa Manyara.Pia kuongeza vyanzo vipya vya ukusanyaji mapato ya ndani, ambapo halmashauri itaanza kukusanya mapato katika vyanzo vyake vipya vya mapato.Itaboresha miundo mbinu ya minada ili kuzuia ukwepaji wa ushuru na kuanzisha minada mipya,vilevile kuendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za uchangiaji miradi ya maendeleo.
Katika kikao hicho bajeti ya shilingi 33,432,375,089 imepitishwa.Mapato ya ndani yakiwa ni shilingi 2,179,069,168, mishahara shilingi 22,432,026,741, miradi ya maendeleo 7,865,880,180 na matumizi mengineyo (OC) 955,399,000.
.................MWISHO......................
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa