BVR Kit Opareta Akiboresha Taarifa za Mpiga Kura Kituo Kikuu cha Wilaya, Kata ya Kibaya
Mwandikishi Msaidizi Akimkabidhi Fomu Mama Aliyefika Kituoni Hapo Kuboreshaji Taarifa Zake Katika Daftari la Wapiga Kura Kituo Kikuu cha Wilaya ya Kiteto, Kibaya
Uboreshaji huo ulioanza tarehe 17.06.2020 na kumalizika leo tarehe 20.06.2020 katika kituo kimoja tu ambacho ni kwa Wilaya nzima ya Kiteto Kata ya Kibaya. Hii imewapa haki ya kikatiba wananchi wote fursa ya kurekebisha taarifa zao ili waweze kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba 2020. Kwa awamu hii hakukuwa na uandikishaji mpya.
Baadhi ya mambo ya msingi yaliyozingatiwa kwa sasa ni pamoja na urekebishaji wa majina ya mpiga ya mpiga kura kama hayakuchapishwa kwa usahihi na kumfuta mpiga kura kwa sababu mbalimbali zinazokubalika kisheria kama vile mpiga kura aliyefariki.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa