Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Queen Cuthbert Sendiga amesema kwamba suala la uboreshaji wa miundombinu katika serikali ya awamu ya sita ya Mhe Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni suala endelevu.
Hayo ameyasema Agosti 16,2023 katika ziara yake maalumu Wilayani Kiteto wakati akiweka jiwe la msingi katika daraja la Orkine lililopo kata ya Songambele.
Mh Sendinga amesema kwamba, katika uboreshaji wa miundombinu ya barabara licha ya kuwasaidia wananchi kupita kwa urahisi ila pia inasaidia ufufuaji wa uchumi wa wananchi wa maeneo hayo.
Mbali na uwekaji wa jiwe la msingi katika daraja hilo, Mh Sendiga ameongoza zoezi la upandaji miti kando kando ya daraja hilo ili kutunza na kuhifadhi mazingira ya eneo hilo la daraja.
Pia Mh Sendiga pia ameweka jiwe la msingi katika Shule ya Msingi Azimio iliyopo katika kata ya Matui wilayani hapo. Shule hiyo ambayo inatarajiwa kufunguliwa na Mwenge wa Uhuru Oktoba 7,2023, inajengwa kwa gharama ya shilingi 540,300,000 kupitia mradi wa BOOST.
Katika kuhitimisha ziara yake wilayani hapo, Mh Sendiga amefanya mkutano wa hadhara katika kituo cha mabasi Matui ili kuongea na wananchi na kusikiliza kero zao.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa