Septemba 2,2024 Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto imefanya kikao na Viongozi wa Dini, Wazee Maarufu pamoja na wawakilishi wa wananchi ajenda kuu ikiwa ni kutangaza tarehe ya Zoezi la Uboreshwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mbali kutangazwa kwa tarehe hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Remidius Mwema amewaomba viongozi wao kushirikiana na serikali katika kuhamasisha waumini wao/wanaowangoza kushiriki katika zoezi hilo muhimu kwani viongozi hao wananafasi kubwa kwa watu wanaowaongoza.
Aidha katika kikao hicho, Afisa Uchaguzi Wilaya, Ndg. Regina Loosurutia alitaja sifa za wahusika wa uboreshaji wa taarifa na sababu za kutoandikishwa kuwa mpiga kura.
Aidha, Afisa Uchaguzi huyo alitumia jukwaa hilo kutangaza pia tarehe ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambayo ni Novemba 27,2024.
Nae Mkuregenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, CPA. Hawa Abdul Hassan amewashukuru viongozi hao kwa kuitikia wito wa kikao hicho na kuwaomba ushirikiano wao.
Zoezi la Uboreshwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Wilaya Kiteto linatarajiwa kuanza Septemba 25, 2024 hadi Oktoba 1,2024. Wilaya ina jumla ya vituo vya uandikishaji 214.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa