Wajumbe wa Kamati ya Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Wakisikiliza Maelezo Mbalimbali ya Mradi Huu Toka kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kijungu tarehe 23.08.2019
Mradi wa Ujenzi wa Vyumba Viwili (2) vya Madarasa Ambapo Ofisi ya Mkurugenzi Imejenga Madarasa Matatu (3) kwa kiwango bora na thamani ya fedha ya Tshs. 46,000,000/=. Kama Yanavyoonekana Hapo Juu katika Shule ya Msingi Kijungu Kata ya Kijungu Halmashauri ya Wilaya Kiteto.
Ujenzi wa Choo Matundu Sita (6) Shule ya Msingi Kijungu
Mradi wa Ujenzi wa Vyumba Viwili (2) vya Madarasa Ambapo Ofisi ya Mkurugenzi Imejenga Madarasa Matatu (3) kwa kiwango bora na thamani ya fedha ya Tshs. 46,000,000/=. Kama Yanavyoonekana Hapo Juu katika Shule ya Msingi Mbikasi Kata ya Sunya Halmashauri ya Wilaya Kiteto.
Mradi wa Ukamilishaji Ujenzi wa Vyumba Viwili (2) vya Madarasa Ambapo Ofisi ya Mkurugenzi Imejenga Madarasa Matatu (3) kwa kiwango bora na thamani ya fedha ya Tshs. 25,000,000/=. Kama Yanavyoonekana Hapo Juu katika Shule ya Msingi Kiteto Kata ya Laiseri Halmashauri ya Wilaya Kiteto.
Ukamilishaji wa Ujenzi wa Chumba 1 cha Darasa na
Kupaua Chumba 1 cha Darasa Shule ya Msingi Ukombozi Kata ya Engusero Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa Shule ya Msingi Makame Kata ya Makame Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
Mradi wa Ukamilishaji Ujenzi wa Vyumba Viwili (3) vya Madarasa Kama Yanavyoonekana Hapo Juu katika Shule ya Sekondari Loolera Kata ya Loolera Halmashauri ya Wilaya Kiteto.
------------------------------------------------ HABARI KAMILI ------------------------------------------------
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ilifanya ukaguzi wa miradi tarehe 23-24.08.2019 katika Kata 17 ambazo ni Makame, Njoro, Olboloti, Chapakazi, Dosidosi, Bwawani, Matui, Namelock, Kaloleni, Bwagamoyo, Loolera, Kijungu, Lengatei, Sunya, Laiseri, Magungu, na Engusero.
Kiujumla Hali ya Utekelezaji wa Miradi ni mzuri sana kwa kuangalia ubora wa majengo husika, gharama ndogo ukilinganisha na bajeti ilopangwa na idadi kubwa ya vyumba vya madarasa kutoka 19 yaliyotarajiwa lakini yamejengwa madarasa 32 yaani ni sawa na ongezeko la 40.6% kwa madarasa 13 yaliyoongezeka kwa thamani ile ile ya 593,735,221/= Miradi mizuri zaidi ni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa Katika Shule za Msingi Makame, Chekanao, Azimio, Bwawani, Kijungu, Mbikasi, na ujenzi wa mabweni na vyumba vya madarasa katika Shule ya Shule ya sekondari Kiteto.
Wachangiaji wa fedha hizi za miradi ni Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kwa kutumia mapato ya ndani (Own source) na wadau wengine ikiwamo Serikali kuu, Mfuko wa jimbo, Taasisi ya Elimu Tanzania, Benki ya NMB na mradi wa EP4R wa Tanzania.
Wananchi wa Wilaya ya Kiteto wanafuraha baada ya kuona utekelezwaji wa miradi hii katika Kata zao kwa vitendo itawasaidia kuondoa kero mbalimbali za kielimu hususani kupunguza msongamano wa wanafunzi itakayopelekea kuongeza ufaulu wa wanafunzi ambapo anayefaidika ni mwananchi husika.
Kamati inaunga mkono matumizi ya (force account) ili kuongeza tija ya kutekeleza miradi mingi zaidi, usimamizi wa dhati wa miradi husika na kuongeza juhudi ya kukusanya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya hii itapelekea kuongeza wigo zaidi wa kuongeza miradi mingine kwa wananchi.
Nawasilisha.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa