Leo tarehe 22.04.2017 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (W) Kiteto Bw.John Malle (aliyeshika Mic) amezindua Mnada wa Njoro ulioko Kata ya Njoro umbali wa Kilometa 17 toka Makao Makuu ya Wilaya ya Kiteto (Kibaya Mjini). Kushoto ni Mheshimiwa Diwani Jimbo N. Maitei wa Kata ya Njoro.
Kwa juhudi za Halmashauri (W) kusukuma gurudumu la maendeleo ya Wilaya na Wananchi wake imesimamia kwa dhati kwa kushirikiana na wananchi wa Kata husika hadi kupata eneo hili la ekari kumi (10)
kwa ajili ya shuguli za Mnada, huku uwekezaji wa miundombinu ya Barabara, Maji, Choo kikubwa na kisafi, Jengo zuri la Machinjio linalojitoshereza,
Ulinzi mahususi wa Askari Polisi kwa usalama wa raia na mali zao upo muda wote.
Vitu mbalimbali vya kuuzwa na kununua vinapatikana hapa kuanzia Mifugo (Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo, Kanga, Kuku wa kienyeji wapo kwa wingi), mazao (Mahindi, Alizeti, Mbaazi, Mtama na Ulezi), Matunda, bidhaa mbalimbali za madukani zinapatikana kwa uhalisia wa gharama utakayoimudu basi ukisoma taarifa hii karibu Kiteto, karibu Mnada Mpya wa Njoro kila Jumamosi ya kila wiki.
Kutoka kushoto mwenye nguo ya rangi nyeupe ni Mshereheshaji Bw. Kimolo, wa pili ni Mhasibu wa Mapato (W) Bw. C. Mwigani,
wa tatu aliyeshika Mic ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (W) Kiteto Bw.John Malle akihutubia wananchi waliofika Mnadani hapo.
Lengo la Kuwepo kwa Mnada huu
kuongeza wigo wa eneo la watu wengi kuweza kufanya biashara,
Kuweka msingi wa kuimarisha masoko ya uchumi wa viwanda utakaokuwa na bidhaa nyingi.
Faida Kuwepo kwa Mnada huu
Kuongeza ajira katika jamii yetu kupitia kushiriki katika biashara na utoaji huduma mbalimbali,
Kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na familia kwa ujumla.
Kurahisisha upatikanaji wa vyakula na huduma zingine muhimu.
Kwa ujumla wake yote haya hupelekea kuwa na maisha bora kwa kila Mtanzania.
Wananchi wakimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (W) Bw.John Malle kwa kumpigia makofi na kunyanyua mikono juu
ikiwa ni ishara ya kupokelewa vyema na kukubalika
uanzishwaji wa Mnada huu ambao ni chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii Kata ya Njoro na Kiteto kwa ujumla.
Afisa Mtendaji Kata ya Njoro Bibi Mariam akiwasalimia wananchi.
Katika uzinduzi huu Kaimu Mkurugenzi huyo amesisitiza mambo ya msingi yafuatayo:-
- Wananchi kujituma katika kufanya kazi kwa bidii siku zote ili kujiletea maendeleo ya mtu binafsi, kaya na Taifa kwa ujumla
- Kila mfanyabiashara kutumia busara katika kufanya biashara hapa mnadani bila kuanzisha tabia mbaya za vurugu, uwizi na
vinginevyo vinavyofanana na hivi ili kuinua hali ya kibiashara ambayo itatunufaisha sisi wote.
- Kila mtu aliyefika hapa leo awe mwakilishi mzuri wa kuutangaza mnada huu ndani na nje ya Wilaya ya Kiteto ili uendelee kukua.
Mifugo aina ya Kondoo katika mauzo
Mifugo aina ya Mbuzi katika mauzo
Mifugo aina ya Ng'ombe katika mauzo
Kuku ambao mteja ameshawanunua amewaning'inIza anaondoka nao kwa Pikipiki maarufu "boda boda" kwenda nyumbani kwa biashara na kitoweo pia.
Mazao mbalimbali
Nyama Choma za Minadani
Nguo mbalimbali
Vyombo mbalimbali kwa matumizi ya nyumbani
Bidhaa mbalimbali
Machinjio nzuri na kubwa ya Mnadani hapo.
Choo kikubwa na kizuri cha kulipia
Watoa huduma ya usafirishaji nao hawako nyuma katika kujipatia riziki kupitia usafirishaji wa abiria na uchukuzi wa mizigo, Taxi, Pikipiki maarufu Bodaboda zote zinapatikana hapa.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa