Vijana wilayani Kiteto wameaswa kuacha kukaa vijiweni pasipo na kazi na kujiunga kwenye vikundi ili waweze kunufaika na mikopo inayotelewa na halmashauri.
Rai hiyo imetolewa Julai 13,2025 na Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa , Ndg. Ismail Ali Ussi mara baada ya kutembelea mradi wa kikundi cha vijana Weredi Studio.
Kikundi cha Vijana Weredi Studio ni moja ya vikundi 39 vya vijana ambavyo vimenufaika na mkopo wa 10% kutoka halmashauri ambapo vikundi hivyo vyote vimepokea mkopo wenye thamani ya zaidi ya milioni 111.
Kikundi hiki kilinufaika na mkopo wa shilingi milioni 10 ambayo iliwasaidia kufanya ukarabati wa studio na pia iliwasaidia kuongeza mtaji ambapo walinunua vitendea kazi.
Upatikanaji wa mkopo kwa kikundi hicho, umewawezesha vijana hao kufanya kazi kwa ufanisi na kuwawezesha kufanya kazi ndani na nje ya wilaya hivyo kujiongezea kipato na kuzalisha ajira kwa vijana wenzao.
Aidha kikundi hicho kimeanza kuelimisha vijana wengine kuhusu kujiunga kwenye vikundi ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kuachana na dawa za kulevya na tabia hatarishi.
Katika mwaka wa fedha 2024/2025 halmashauri imeweza kutenga zaidi ya shilingi 279 kwaajili ya kuwawezesha kiuchumi vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye walemavu na kiasi hicho chote kilishawekwa kwenye akaunti maalumu ya vikundi vya makundi hayo.
Ndg. Ussi ameipongeza halmashauri kwa juhudi wanayofanya ya kutenga fedha kwaajili ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kutekeleza miradi ya kiuchumi .
Aidha aliwahimiza vijana kujiunga kwenye vikundi ili waweze kunufaika na mpango huo.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa