Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Emanuel Mwagala (aliyesimama) Akifungua Kikao cha Kamati ya Lishe Jana tarehe 03.02.2020 Kilichofanyka Katika Ukumbi wa Jengo la Utawala Katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto.
Idara na Sekta Mbalimbali Wakiwasilisha Taarifa Zao Katika Kikao Hicho.
Picha za Wajumbe Mbalimbali wa Kikao
Kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kiteto, Bi.Beatrice Rumbeli Akiendesha Kikao
Kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kiteto Bi.Beatrice Rumbeli Akiahirisha Kikao.
---------------------------------------------------------- HABARI KAMILI -------------------------------------------------------------
Hayo yamejiri jans tarehe 03.02.2020 katika kikao cha lishe cha robo ya pili kilichofanyika katika ukumbi wa jengo la utawala, Hospitali ya Wilaya ya Kiteto. Katika kikao hicho imefahamika kuwa Serikali inatoa leseni kwa wananchi wote wenye viwanda lakini hii ni baada ya kujuridhisha katika mambo kadhaa yanayohusiana na kiwanda husika ikiwa ni kwa maslahi mapana ya mwenye kiwanda na walaji kwa ujumla wao.
Kamati ya chakula na dawa ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kwa kushirikiana na ofisi ya Afya usafi na Mazingira wanamalaka kisheria kutoa elimu na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika viwanda hivi na kumshitaki yeyote anayeenda kinyume na utaratibu wa serikali.
Hata hivyo kamati za wazazi zinazochangisha na kupokea chakula mashuleni zimehimizwa kuwa makini katika vigezo vya uagizaji na upokeaji wa vyakula husika na kukagua kabla ya kupokelewa na pia kuhifadhiwa na uandaaji wake hadi kuwa chakula ili kulinda afya za wanafunzi hao ambao taifa linawategea kama nguvu kazi ya siku za usoni.
Wazazi wanaendelea kuhimizwa kuchangia chakula kwa ajili ya faida endelevu ya kimwili na kiakili kwa watoto wao wenyewe kwani mtoto atapata lishe bora ambayo kwa umri wa mtoto alionao ni msingi mzuri sana wa kuimarika kiafya ambapo maisha yake yote hujengwa msingi imara wa kutodumaa huku akili yake inakuwa tayari kwa kusoma muda wote hivyo hatapoteza muda wa masomo katika kutembea kwenda nyumbani, matokeo yake ni kupandisha ufaulu wa watoto wetu ambao kwa baadaye ndiyo wataalamu tunaowategemea katika familia na taifa kwa ujumla wake kwenye fani mbalimbali za sayansi, biashara na sanaa kama vile udaktari, uhandisi, kompyuta na zingine nyingi.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa