• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

''Vyakula vya Shule Visinunuliwe kwa Zabuni’’ - RC Mnyeti

Imetumwa : February 5th, 2018


Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Mhe.  Alexander Mnyeti  Akiwasalimia Wanafunzi wa Shule  ya Msingi Partimbo katika  Ziara  Yake Shule ya Msingi Partimbo.

  Wanafunzi wa  Bweni Katika Shule ya Msingi Partimbo Wakipiga Makofi kama Ishara ya Kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Mhe. Alexander Mnyeti Alipotembelea Shule Hiyo.

 Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Mhe.  Alexander Mnyeti Akitoa Maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa Katika  Ziara  Yake Shule ya Msingi Partimbo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Ndg. Tamim Kambona Akifafanua Jambo Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Mhe.  Alexander Mnyeti  Katika  Ziara Shule ya Msingi Partimbo.

Mwalimu Mkuu wa  Shule ya Msingi Partimbo  Mwl. Donald Mazengo  Akiwasilisha Taarifa ya Shule Yake Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Mhe. Alexander Mnyeti ,Wakati wa Ziara ya Mhe. Mnyeti Katika  Shule Hiyo.

Majengo ya shule ya sekondari Partimbo ,Shule ambayo  Ujenzi Wake Ulianzishwa  kwa Fedha Zilizochangwa na  Wananchi wa Kata ya Partimbo.



.............HABARI KAMILI...........



''Vyakula  vya Shule Visinunuliwe kwa Zabuni’’ - RC Mnyeti

Mkuu wa mkoa wa Manyara mheshimiwa Alexander Mnyeti amewataka wakuu wa shule kuacha kununua vyakula vya shule kwa zabuni, badala yake wanunue kwa bei ya soko ili kupunguza gharama.Mheshimiwa Mnyeti ameyasema hayo akiwa katika  ziara yake katika shule ya msingi partimbo, iliyopo kata ya Partimbo wilayani Kiteto ,baada ya mkuu wa shule hiyo mwalimu Donald  Mazengo kueleza changamoto zinazoikabili shule hiyo ikiwemo upungufu wa fedha za chakula ambapo shule hiyo  inapata shilingi 8,331,529 kwa mwezi , idadi ya wanafunzi wa bweni ikiwa ni 265.Na hivyo kuwa na upungufu wa takribani shilingi milioni tano .


Kabla ya kujibu kuhusu changamoto hiyo Mhe. Mnyeti  akataka maelezo kutoka kwa kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara ndugu Anold Msuya . Hapa Msuya anasema ‘‘Ni kweli shule hii inapata kiasi hicho cha fedha, lakini tulishatoa maelekezo ambayo yalitolewa na  TAMISEMI, na tulileta  hapa halmashauri kwamba kamati za shule zitanunua chakula.Kwa hiyo wajitahidi kununua chakula kwa bei ya soko na sio kwa zabuni.Wakifuata utaratibu huo,wakinunua chakula wakati wa mavuno ,watanunua kwa bei ndogo,kwa hiyo chakula kile kitachukua muda mrefu kuliko ambavyo kingenunuliwa na wazabuni’’.  Baada ya majibu ya katibu Tawala wa Mkoa Mhe. Mnyeti akauliza kuhusu utaratibu unaotumika kununua chakula shuleni hapo ambapo mwalimu Mazengo alijibu kwamba chakula kinanunuliwa kwa zabuni, ndipo Mhe. Mnyeti akatoa tamko kwamba vyakula visinunuliwe kwa zabuni,badala yake wakuu wa shule wanunue vyakula wenyewe.Akisisitiza kuhusu tamko hilo Mhe. Mnyeti anasema “kununua vyakula kwa zabuni ni gharama kubwa sana, hivyo fedha inayotolewa na serikali kwa ajili ya chakula kwa mwezi haiwezi kutosha.Lakini  mwalimu mkuu ukinunua vyakula mwenyewe kwa bei ya soko fedha hizo zinatosha sana.Kwa watoto 265 ,shilingi 8,331,529 kwa mwezi  zinatosha kabisa, kama utanunua vyakula mwenyewe.Hakikisha watoto wanakula wanashiba ,nunua mwenyewe vyakula’’.


Aidha Mhe. Mnyeti akataka ufafanuzi kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Tamimu Kambona kwa nini  vyakula vya shule  vinanunuliwa kwa zabuni , hali ya kuwa maelekezo  kuhusu manunuzi ya vyakula hivyo yalishatolewa. Hapa Mkurugenzi Kambona anatoa ufafanuzi anasema ‘‘ tulishawaambia kwa mwaka huu kwamba utaratibu ni huo ,lakini tuliwaambia tukiwa tumechelewa.Na mimi mwenyewe ndiye niliye gundua tatizo ,ambapo  kule Ndedo tulikuta chakula cha zabuni  kinauzwa  gunia moja la unga shilingi 200,000 ,nikaja kufuatilia mchakato wote kujua nini kilitokea,baadae tukawaagiza wazabuni wote  wakae  bei  hizo zishuke.Tulipambana sana , bei ya gunia la unga ikatoka kwenye shilingi  200,000 ikashuka hadi 120,000 , na vitu vingine pia vikaendelea kupunguzwa bei. Lakini na mimi niliagiza niliwaambia kwamba kuanzia sasa zoezi hili la kutumia wazabuni life.Nataka wakuu wa shule wanunue vyakula wenyewe”.


Changamoto nyingine zinazoikabili shule ya msingi Partimbo  ni uchakavu wa majengo, ukosefu wa umeme na kutokuwa na uzio . Kuhusu changamoto ya shule hiyo kutokuwa na uzio, mwalimu Mazengo amemueleza Mhe. Mnyeti kwamba kutokana na shule hiyo kutokuwa na uzio walimu wanapata shida sana kuwadhibiti wanafunzi  kwa sababu wanafunzi hao huchukuliwa kutoka sehemu mbalimbali ambapo sehemu hizo wazazi hawapendi watoto wao waende shule,hivyo kutokana na kutokuwa na uzio kuna wazazi wanakuja kuwatorosha wanafunzi, na wanafunzi wengine hutoroka wenyewe,lakini kama kungekuwa na uzio wangeweza kuwadhibiti .Akijibu kuhusu changamoto hiyo  Mhe. Mnyeti  anasema “ Mkurugenzi anza na hili la uzio.Hii shule ipe kipaumbele kwa sababu watoto wanaweza wakazidi zaidi ya hapo.Wale wote wanaohangaika huko vijijini wakiletwa hapa hii shule itakuwa kubwa sana,sasa sio lazima ufanye kwa mara moja ,anza ujenzi kwa awamu kulingana na uwezo wa halmashauri.Kama ulivyofanya pale hospitali,umefanya kazi kubwa sana .Uwezo wako tunauona ,na tunaujua ,sasa hebu fanya na hapa walimu wanapata shida ,unaweza kuwasaidia kwa kuwajengea ukuta”.


Kuhusu changamoto ya uchakavu wa majengo , Mhe.Mnyeti alimtaka Mkurugenzi  kutoa majibu ,na hapa mkurugenzi anasema “ Suala la ukarabati tumeanza ,hizi shule za bweni ziko saba,tulianza  na shule ya Kibaya na kule Ndedo .Hii shule iko kwenye bajeti  kwa mwaka huu wa fedha tunaoendelea nao.Tunategemea wakati wowote fedha za ruzuku ya maendeleo (LGDG) zikiingia tutakuja kufanya ukarabati wa majengo katika shue hii”.


 Kwa upande wa changamoto ya kutokuwepo kwa umeme katika shule hiyo. Mhe. Mnyeti amemtaka katibu tawala wa mkoa kumuandikia barua meneja wa TANESCO wilaya ya Kiteto  atume wataalamu wake katika shule hiyo, wafanye tathimini, waseme nini kinahitajika ili umeme uweze kufika shuleni hapo wanafunzi wa bweni wanaosoma katika shule hiyo wasiendelee kukaa gizani.


Wakati huohuo Mhe. Mnyeti amefanya ziara  katika shule ya sekondari Partimbo  ambapo amewapongeza wananchi wa kata ya Partimbo kwa kuweza kuanzisha  ujenzi wa shule ya sekondari katika kata yao na  kumtaka ndugu Msuya ambaye ndiye afisa elimu Mkoa kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapangwa kwenda kusoma katika shule hiyo na vilevile walimu wapangiwe kufundisha katika shule hiyo, ili ianze kufanya kazi mara moja,wananchi wasiendelee kuona kwamba nguvu zao zimepotea bure. Akisisitiza kuhusu kuanza kazi kwa shule hiyo Mhe. Mnyeti anasema “ wananchi wanapoanzisha miradi ya maendeleo ni vema miradi hiyo ikasimamiwa na kuanza kufanya kazi zilizokusudiwa ili wasione kwamba wamepoteza nguvu zao. Watieni moyo wananchi kwa kuleta walimu na wanafunzi katika shule hii, ufundishaji uanze mara moja”.


Shule ya sekondari Partimbo ilianza kujengwa mwaka 2010 kwa nguvu za wananchi, ambapo wananchi hao walichangia shilingi 11,000,000 na kufanikiwa kukamilisha ujenzi wa madarasa matatu.Halmashauri ya wilaya ya Kiteto kupitia fedha za ndani za halmashauri shilingi 10,000,000 ,fedha za elimu ( Perfomance for Result) shilingi 11,000,000 , fedha za mfuko wa jimbo shilingi 13,000,000 na fedha za ruzuku ya maendeleo shilingi 20,000,000 ( LGDG) imejenga madarasa mawili, maabara mbili , moja ya somo la kemia na nyingine ya somo la baiolojia, maktaba  pamoja na vyoo; choo cha wanafunzi  chenye jumla ya matundu nane na choo cha walimu, matundu mawili .Hadi sasa madarasa matano na maabara moja ya somo la baiolojia ujenzi wake umekamilika, maabara moja ya somo la kemia, maktaba pamoja na vyoo viko katika hatua ya umaliziaji ( finishing).



...............MWISHO...............

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa