Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Kiteto, CPA. Hawa Abdul Hassan amewaomba wadau wa siasa wilayani hapo kushirikiana na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi katika uhamasishaji wa zoezi la Uboreshwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Rai hiyo imetolewa Septemba 13,2024 katika kikao na Makatibu wa Vyama vya Siasa, chenye lengo la kuwashirikisha wadau hao kuhusu zoezi hilo.
Katika kikao hicho Afisa Mwandikishaji huyo mbali na kuwapa taarifa juu ya maandalizi ya zoezi hilo, Afisa huyo amewaeleza wadau hao kuwa kufanikiwa kwa zoezi hilo pia kunategemea ushiriki wa vyama vya siasa na hivyo aliwaomba wadau hao kutoa ushirikiano.
Mbali na hayo, CPA. Hawa amewaambia Makatibu hao wa vyama vya siasa kuandaa mawakala kutoka katika vyama vyao kwaajili ya usimamizi wa zoezi hilo.
"Jimbo letu lina vituo vya uandikishwaji 214, ikiwapendeza tunaomba tupate mawakala kwenye kila kituo", ameongeza CPA. Hawa.
Zoezi la Uboreshwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Jimbo la Kiteto, litaendeshwa kwa siku saba kuanzia Septemba 25 hadi Oktoba 1,2024
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa