Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhe. Remidius Mwema Emmanuel Agosti 15, 2025 amekabidhi jumla ya mizinga 65 ya kisasa ya nyuki kwa jamii ya Akie wanaoishi katika maeneo ya Kinua kata ya Namelock, ikiwa ni hatua ya kuwawezesha kiuchumi na kuimarisha ustawi wao wa kijamii.
Mizinga hiyo imetolewa na Shirika la Kijamii la Ujamaa Community Resource Team (UCRT) kwa kushirikiana na wafadhili wake, Inclusive Conservation Initiative (ICI), ambalo linafanya kazi ya kutunza mazingira na kusaidia jamii asili kupata mbinu mbadala za kujipatia kipato.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, DC Mwema amelishukuru shirika hilo kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kuibua fursa za kiuchumi kwa wananchi, hususan jamii ya Akie ambayo kiasili imekuwa ikitegemea uwindaji, kuokota matunda na urinaji wa asali kama njia kuu za maisha.
Aidha, amewataka wananchi hao kutumia mizinga hiyo kwa bidii na ubunifu ili kuboresha kipato chao, kulinda mazingira na kuendeleza mila na tamaduni zao ambazo ni sehemu ya urithi wa taifa.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa