Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Emanuel Mwagala (aliyesimama) Akifungua Kikao cha Kamati ya Lishe Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
Dkt. Mwanaidi Shaban Akitoa Salamu kwa Wajumbe wa Kamati Ikiwa ni Pamoja na Kumkaribisha Mwenyekiti wa Kikao Bw. E. Mwagala
Wajumbe mbalimabli katika kikao hicho
Bw. Pundugu Balabala akiwasilisha taarifa ya Idara ya Kilimo na Umwagiliaji kwa niaba ya Afisa Kilimo na Umwagiliaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
Bw. Emanuel Masha akiwasilisha taarifa ya Idara ya Mifugo na Uvuvi kwa niaba ya Afisa Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
Bi. Fatuma Kawia Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto akiwasilisha taarifa.
Bi. Amina Mwesa akiwasilisha tarifa ya Idara ya Maji (kwa sasa RUWASA wakala wa Maji Mjini na Vijijini) kwa niaba ya Meneja wa RUWASA Wilayani Kiteto.
Bw. Rodrick Kidenya Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto akiwasilisha taarifa.
Bw. Mohamed Ismail mwakilishi wa Wamiliki wa Mashine za Kukamua Alizeti Wilayani Kiteto akiwasilisha taarifa.
Bw. Fabian Simon akiwasilisha tarifa ya Idara ya Elimu Sekondari kwa niaba ya Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
Bw. Seif Lipyoga akiwasilisha taarifa ya Idara ya Afya Kiteto cha Madawa niaba ya Mfamasia wa Halmashauri ya Wilaya ya KitetoBw. Godwin Nagolo akiwasilisha taarifa ya Asasi Isiyoya Kiserikali (NGO) ya Mwanasatu Development Organization (MWADO) Wilayani Kiteto.
Bw. James Paul akiwasilisha taarifa ya Idara ya Mipango kwa niaba ya Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
Bw. Kerevatus Sibanganya akiwasilisha taarifa ya Idara ya Usafi na Mazingira kwa niaba ya Afisa Usafi na Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
Mwakilishi wa BAKWATA Wilayani Kiteto Bw. Ibrahim Bori akichangia mada.
Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bi. Beatrice Lutanjuka akichangia mada kwenye kikao hicho.
-------------------------------------- HABARI KAMILI -----------------------------------------
Haya yamejiri katika kikao cha Kamati ya Lishe Wilayani Kiteto Julai 2019 ambapo Idara, Vitengo na Wadau wengine wa afya ya lishe kama zilivyotajwa hapo juu kwenye mawasilisho walijadili. Ili kuwa na lishe bora, kiwango cha ubora wa mafuta ni muhimu sana kwa afya ya binadamu lakini pia mfanyabiashara husika atakua kiuchumi kwani atakuwa amejipatia fursa ya kutosha kwa kupata soko la uhakika ndani na nje ya nchi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti ni kwamba, ukamuaji wa alizeti unafanywa na wafanyabiashara wenye weledi wanaofuata sheria, taratibu na kanuni za Wakala wa Chakula na Dawa nchini (TFDA) pamoja na Shirika la Viwango nchini (TBS) kiasi kwamba wanahakikisha wanakamua alizeti inayoonekana ni nzuri na salama kwani wakamuaji alizeti wanajua kuzitofautisha kuwa zipi ni mbaya na zipi ni nzuri.
Chanzo cha mafuta kuwa mabaya hasa yale machungu hakijajulikana kisayansi kwamba nini hasa kinasababisha haya, lakini kwa uzoefu wa wanaoshugulika na ukamuaji wa alizeti wamesema wamefuatilia kwa kina waligundua sababu kuu mbili; ya kwanza ni kwamba huwa tatizo linaanzia shambani kutokana na alizeti kuvunwa bila kukauka kwa kiwango kinachotakiwa hivyo zikihifadhiwa punje za alizeti husika huvunda na zikikamuliwa mafuta hayo huwa machungu ambapo hizi alizeti ukiziona unazitambua na ukitafuna punje zake ni chungu pia, na la pili ni mafuta ya alizeti yanayopatikana baada ya kuchemsha mabaki ya alizeti yaliyokwisha kukamuliwa viwandani maarufu kama tope.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kupitia Kamati ya Lishe na Kamati ya TFDA ngazi ya Wilaya imesisitiza wamiliki wa mashine hizi za kukamua alizeti bora na atakayeonekana kukiuka agizo hili atachukuliwa hatua kali za kisheria, lakini pia akionekana mtu anazo alizeti za aina hiyo basi itolewe taarifa haraka Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ili hatua za kisheria ziweze kuchukua mkondo wake kwani kuna madhara yanayoweza kutokea kwa walaji aidha moja kwa moja au kuathiri afya za binadamu taratibu. Kamati za ukaguzi wa mashine hizi za kukamua alizeti zinafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha mwananchi anakuwa salama na wadau wote wanaohusika wanafuata miongozo ya TFDA na TBS ipasavyo.
Matokeo chanya ya jambo hili kufanywa hivyo kutakuwa kunaisaidia jamii kupata lishe bora kwa kutumia mafuta bora, na wao kama wafanyabiashara watakuwa katika nafasi nzuri ya kibiashara kwa mafuta husika kuuzwa si tu ndani ya nchi lakini na kimataifa pia, jambo ambalo litakuwa limeongeza wigo wa soko la mafuta yao matokeo yake ni kupata fedha nyingi za kigeni ambazo ni zitaongeza mtaji wa mfanyabiashara mwenyewe, serikali kuongeza makusanyo mbalimbali yanayotokana na uzalishaji huu kupitia kodi, manunuzi ya umeme, maji na vifungashio. Pia kutaongeza mnyororo wa ajira katika sekta ya kubwa ya kilimo bila kusahau usafirishaji na kuongezeka kwa ubunifu wa teknolojia tatuzi ya uzalishaji itakayotokana na mahitaji mvuto "demand driven" ya ushindani wa kimataifa.
Akizungumza wakati wa majadiliano, Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bi. Beatrice Lutanjuka amesema Sumukuvu bado ni changamoto, jamii bado haina uelewa wa kutosha katika kuhifadhi mazao yao hususani nafaka kama mahindi, karanga na mtama ili mazao hayo yasiweze kupata sumukuvu, jambo ambalo ni hatari sana kwani madhara ya sumukuvu ni makubwa. Sumukuvu inapoingia mwilini kidogo kidogo, madhara yake hayawezi kuonekana kwa mara moja, lakini moja wapo ya madhara yanayoweza kuonekana baada ya muda mrefu ni saratani ya ini.
Wataamu wa Mifumo na Uvuvi wamefafanua zaidi kuhusu sumukuvu, kwamba Sumukuvu haiko kwenye nafaka peke yake, bali inaweza kuwepo hata kwenye nyama, pamoja na mazao ya mifugo kama vile maziwa, kutokana na mifugo kula vyakula ambavyo vina sumukuvu, hivyo jamii inapaswa pia kutahadharishwa kwamba mifugo inapokula mabua au pumba ambazo zina sumukuvu, nyama pamoja na mazao yake yote ambayo hutumika kama chakula kwa binadamu vyote vinaweza kuwa na viambata vya sumu hiyo.
Nawasilisha.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa