• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Wakazi wa Kiteto Watakiwa Kuchukua Tahadhari Kuhusu Ulaji wa Nyama

Imetumwa : January 16th, 2018

                                    Daktari wa Mifugo Wilaya ya Kiteto  Dkt. Lunonu Sigala akielezea kuhusu ugonjwa wa mifugo  unaosababisha mifugo mingi kufa wilayani Kiteto.

                            Pichani ni mabaki ya nyama ambayo imetokana na mifugo iliyochinjwa baada ya kufa. Ulaji wa nyama hizi ,na mazingira haya ya upatikanaji wake ,ndio chanzo cha mlipuko wa ugojwa wa kuharisha na kutapika katika baadhi ya vijiji  wilayani Kiteto.


                Hali ilivyo sasa katika baadhi ya maeneo  ya wafugaji wilayani Kiteto ambapo mifugo imekuwa ikianguka na kufa na wafugaji kuacha mizoga ikizagaa, kitu ambacho ni hatari sana kwa afya za binadamu na viumbe hai wengine. 

( Picha zote ni kwa hisani ya idara ya afya mazingira na idara ya mifugo wilaya ya Kiteto)


                                                                                                             ............... HABARI KAMILI..............


Wakazi wa Kiteto Watakiwa Kuchukua Tahadhari  Kuhusu  Ulaji wa Nyama

Wakazi wa wilaya ya kiteto mkoani Manyara  wametakiwa kuchukua tahadhari kuhusu ulaji wa nyama ambayo haijakaguliwa na wataalamu wa mifugo, pia kuhakikisha  kwamba nyama inahifadhiwa na kuandaliwa vizuri na kwa umakini  kabla ya haijaliwa. Tahadhari hiyo imetolewa  na Afisa afya  mazingira  wilaya ya Kiteto ndugu Israel Nyalubeli kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa kuharisha na kutapika ambao umevikumba  vijiji vya Krash, Ndirgishi visimani na Taigo vilivyopo katika kata ya Ndirgishi na kijiji cha Emarti kilichopo katika kata ya Magungu. Nyalubeli  amesema kwamba ugonjwa huo  unatokana na kula nyama ya mifugo ambayo imeugua ugonjwa unaosababishwa na kupe  jina la kitaalam Ndigana baridi ( Anaplasmosis) .


Akitoa taarifa  ya mlipuko  wa ugonjwa  huo  Nyalubeli amesema kwamba dalili za wagonjwa wote waliougua kutokana na kula nyama hizo ni kuharisha na kutapika ,dalili ambazo zinafanana na dalili za kipindupindu. Ambapo amesema kwamba  hadi sasa jumla ya watu 43 wameugua ugonjwa huo , na watu 5 wamefariki. Nyalubeli ameanisha  mambo  matatu ambayo yanaweza kuwa chanzo cha ugonjwa huo , ambapo amesema kuwa jambo la kwanza ni nyama kutohifadhiwa vizuri ,ambapo inakuwa ni  mazalia  mazuri sana ya wadudu , wadudu hao  hutengeneza sumu, sumu ikishakuwepo kwenye  nyama , hata ipikwe vipi  haiwezi kwisha, hivyo yeyote atayekula nyama hiyo atapata madhara. Jambo la pili ni  nyama  kutoandaliwa vizuri, Nyama isipoandaliwa vizuri  wadudu hai wanaokuepo kwenye nyama hiyo husababisha madhara kwa mlaji. Jambo la tatu ni mabaki ya dawa kwenye nyama. Dawa hizo zinakuwa  sumu , hivyo binadamu anapokula  nyama hiyo hupata madhara. Hapa Nyalubeli anafafanua zaidi kuhusu  madhara ya kula nyama ambayo imetokana  na mfugo uliogua na kutibiwa kwa dawa nyingi anasema ‘‘Kinachotokea ni kwamba   mifugo inapougua inahudumiwa kwa dawa, na inapokufa dawa hizo zinabaki kwenye  nyama. Kwa hiyo zikifa  ndugu zetu wafugaji  wao wanachojali ni ngozi, wanachuna ngozi kimnyakimnya, na wanajua kabisa kwamba wakila zile nyama zinaweza kuwadhuru kwa hiyo wanachofanya wanauza hiyo mifugo kwa bei nafuu, watu wananunua nyama  wanakula na ndio hapo sasa wanaharisha na kutapika.  Serikali ina utaratibu wa kuyaripoti  haya magonjwa,kwa hiyo ambacho tunajua hadi sasa sampuli za mifugo  zimepimwa, kwa matokeo ya  hapa wilayani  imeonekana ni aina fulani ya wadudu ambao wanatokana na kupe.Lakini kwa sampuli zilizopelekwa wizarani ,mpaka jana tunaongea na dakatari wa mifugo majibu yake yalikuwa hayajarudi.Lakini angalau tunataarifa za mwanzo kwamba chanzo ni hao wadudu.Kwa hiyo tunachokifanya ni kuchukua tu tahadhari kuelimisha watu kwa msisitizo kwamba mizoga isiliwe,mizoga izikwe.Yaani iondoke kabisa kwenye uso wa dunia kwa  sababu ikishaingia kwenye mzunguko wa maji ikaingia kwenye mzunguko wa chakula hakuna atakae kuwa salama na ndio maana sasa tunaenda mpaka kwenye eneo la machinjio , kusimamia ule utaratibu wa kawaida kwamba ng’ombe anakaguliwa siku moja kabla ya kuchinjwa na nyama inakaguliwa baada ya kuchinjwa . Ndio tunawekeza nguvu huko kwa sababu unaweza kushtukia hapa mtu ametoa ng’ombe wake huko anamuona anataka kufa akampigia mchinjaji  njoo ununue kumbe ni kundi lilelile . Kwa hiyo kila mtu yuko kwenye hatari hiyo.Kwa sababu hiyo basi, tumesema kwamba maeneo yote ambayo nyama inaliwa ,wahakikishe kweli ni nyama ambayo imechinjwa ,imekaguliwa na kufuata taratibu zote zinazotakiwa’’.

Kadhalika  Nyalubeli  ameainisha  hatua ambazo zimechukuliwa  na wataalamu wa afya  katika kudhibiti ugonjwa huo .Hatua hizo ni kuchuua historia  kamili ya wagojwa hao kutoka kwa uongozi wa vijiji na familia zilizotoa wagonjwa, kutembelea wagonjwa na kuwapa dawa za kinga tiba , kusimamia na kuhakikisha kwamba wagonjwa wanapelekwa  kituo cha huduma ya afya (Engusero HC)  kwa matibabu zaidi, kuhudhuria mazishi ya  mmojawapo kati ya waliofariki kwa ugonjwa huo na kutoa elimu ya afya  kwenye mazishi;  ya kuwa pindi anapopatikana mgonjwa yeyote  wa kuhara na kutapika akimbizwe haraka kwenye  kituo cha kutolea huduma ya afya. Kwenda kwenye maboma ya wafugaji ambako kulibainika  mifugo iliyokufa  na taarifa ya kuaminika  imedhihirisha kwamba ndio chanzo  cha watu kuharisha na kutapika , kutoa maelekezo kwa uongozi  kwamba ni marufuku watu kula nyama  za mifugo ambayo haijakaguliwa na wataalamu wa mifugo  na wataalamu wa afya , pia kusimamia na kuhakikisha mizoga yote inazikwa  ili kuzuia  kuendelea  kuchafua mazingira na kuhatarisha afya za watu .

Katika hatua nyingine Nyalubeli amesema kwamba  wafugaji wanatakiwa kuzika mifugo yao inapokufa kwani wanapoiacha bila kuizika ni hatari sana, hususani wakati huu wa mvua  ambapo mizoga ya mifugo hiyo inasombwa  na maji na kupelekwa katika vyanzo vya maji, ikizingatiwa hasa kwamba vyanzo vingi vya maji viko katika miteremko, mizoga hiyo isipozikwa ugonjwa huo unaweza kuwapata watu wengi zaidi ambao ni watumiaji wa maji  katika vyanzo ambavyo mizoga hiyo itakuwa imeingia .Akizungumzia mikakati waliyonayo katika kuhakikisha kwamba mifugo hiyo inazikwa Nyalubeli anasema ‘‘tumekubaliana na mkurugenzi  kwamba watendaji wa vijiji wasimamie katika maeneo yao  mifugo inayokufa izikwe ,isiliwe, na barua inayoelekeza hivyo imeshasambazwa  kwa watendaji wote wa vijiji , pia nimezungumza na afisa mifugo wa wilaya  ambaye kwa wakati huu yuko kwenye upigaji chapa ngombe, tumekubaliana kwamba maafisa mifugo wote waambiwe ,ili wanapokwenda kupiga chapa, au kufanya kazi yoyote ile kulingana na majukumu yao  huko  kwenye maboma ,wakikutana na mifugo iliyokufa,wasimamie mifugo hiyo izikwe , na jana tumepeleka matangazo mnadani, kwa sababu pale kuna watu  wengi,tumepeleka matangazo ili  taarifa iwafikie watu wengi.

Kwa upande wake Daktari wa Mifugo Wilaya  ya Kiteto Daktari Lunonu Sigala  amesema kuwa ni kweli kwamba kuna ugonjwa wa mifugo , ugonjwa huo unasababishwa na kupe, kitaalamu unaitwa Ndigana baridi  au Anaplasmosis na umeshaua mifugo mingi sana ,na sababu  kubwa ni kwamba wafugaji hawaogeshi mifugo. Akitoa  uthibitisho wa kitaalamu kuhusu  kuwepo kwa ugonjwa huo wa mifugo wilayani Kiteto  Dkt. Sigala anasema ‘‘ kama Wilaya tumefanya vipimo vyetu ,tumechukua damu kwa ajili ya uchunguzi  wa kimaabara na tumethibitisha kwamba ugonjwa ni huo , na dalili zote asilimia mia moja zinaonyesha hivyo.Kwa hiyo mimi niwatoe hofu wafugaji ,maana wapo watu wanafikiri kwamba ni Kimeta, sio Kimeta, ni ugonjwa wa kupe  unaojulikana kama Ndigana baridi kwa Kiswahili. Kwa hiyo ushauri tunaoutoa  kwa wananchi ni kwamba kama mfugo umekufa wananchi wasile ule mzoga ,wafukie.Na ndio unasikia kuna matukio ya binadamu kuugua na wengine wamefariki  kwa sababu ya kula nyama za mifugo ambayo imeugua ugonjwa huo, kwa sababu mfugo unapo kuwa unaugua anakuwa kwenye tiba, na wafugaji wetu,anachukua dawa hii,akiona hajapona anachukua dawa hii, akiona hajapona anarudi tena kwenye ile dawa ya kwanza anaongeza dozi, kwa kudhani kwamba ile dozi ya mwanzo ilikuwa ndogo, ndio sasa mfugo ukija kufa unakuta ile nyama yote inamabaki ya dawa,kwa hiyo ile ndio inayokuja kusababisha shida sana kwa binadamu. Na hasa ukifuatilia sana waliokufa wote ni wale waliokula maini ya mifugo iliyokufa. Kama tunavyojua kwamba maini ndio kiwanda cha sumu, sumu yote ikishaingia mwilini moja kwa moja inaenda kwenye maini .Kwa hiyo wale walikula kiwango kikubwa sana cha sumu ,na ndio waliugua na hatimaye wengine kupoteza  maisha’’


 Dkt. Sigala amesema kwamba wafugaji hawaogeshi mifugo pamoja na kwamba wanapewa elimu ya kutosha  kuhusu umuhimu wa kuogesha mifugo.Akifafanua kuhusu  sababu ya wafugaji kutoogesha mifugo yao  Dkt. Sigala anasema ‘‘ Tunatoa sana elimu  juu ya umuhimu wa kuogesha mifugo, na kila kijiji tumeunda kamati ya majosho,lakini sijui  hasa  ni nini kinatokea , labda wakati mvua kuna uhaba wa maji kwa baadhi ya vijiji, lakini hata vijiji vyenye mabwawa na pampu walikuwa hawaogeshi mifugo yao. Sasa sijui kama ni sababu za kiuchumi au ni sababu za kijamii kwamba wanahofu na menejimenti ambazo zipo za hayo majosho, lakini hata kwa ngazi ya boma, wanashindwa kuwa na pampu za kuogeshea? Kwa sababu baadhi yao wana pampu za mkono ambazo wanatumia kuogeshea.Kwa hiyo mimi naona bado uzembe ni wa wafugaji. kwa sababu elimu wanayo,na ukirudi kwenye kumbukumbu za miaka miwili nyuma asilimia 75 ya mifugo ya hapa wilayani ilikuwa inaogeshwa, na asilimia tisini ya majosho yalikuwa yanafanya kazi. Lakini sasa hivi kwa kumbukumbu zangu ni kwamba hakuna hata josho moja linalofanya kazi .Sasa hatuwezi kuwa na tatizo linalofanana kwa vijiji  vyote’’.

Akizungumza kuhusu  usimamizi wa majosho  na ufuatiliaji  uogeshaji mifugo Dkt. Sigala  anasema  ‘‘  pamoja na kuwa na kamati za majosho katika vijiji , tuna afisa majosho wa wilaya ambaye kazi yake kubwa  ni kusimamia hayo majosho, na  kuna mwaka kupitia shirika la SNV tulifanya utafiti kwamba ni kwa nini  tabia ya uogeshaji ng’ombe inaenda ikishuka , kijiji kimoja wapo kati ya vijiji tulivyovifanyia utafiti  sababu kubwa ilikuwa ni kwamba kamati nzima ya usimamizi wa josho ilitokea ikawa  ni familia  moja.Kwa hiyo wafugaji wakawa wanaona kwamba kuna jinsi  ambayo fedha zao zinaliwa na hivyo kuacha kuogesha mifugo yao. Kwa hiyo inawezekana suala la usimamizi wa pesa  ni sababu, kwani  kila mahali hali imekuwa hivyo. Nadhani hawana uhakika kwamba fedha wanazolipia kuogesha zinakuwa salama, au zinaliwa, ama zinatumika kweli kufanya shughuli ya kununua dawa tena na kuogeshea . Labda sasa tuone kama serikali tunaweza kuingilia kati hii hali, kwamba sasa turudi kama ilivyokuwa miaka ya sabini  kurudi nyuma ambapo majosho yote yalikuwa chini ya serikali.Lakini hata hivyo uendeshaji wake utakuwa mgumu sana kwa kuwa dawa zote sasa hivi ziko kwenye sekta binafsi’’ .

Aidha   Dkt. Sigara  amesema kwamba  tiba ya kwanza kwa mnyama anapougua ni chakula, akipata chakula cha kutosha ndipo tiba nyingine pia zinaweza kumsaidia kwa haraka. Lakini kutokana na ukame wa miezi michache iliyopita mifugo imekosa chakula na hivyo imekuwa na udhaifu ,ambapo inapotokea inakumbwa na ugonjwa ,inaongezewa na mzigo wa dawa  kali, hali hiyo husababisha mifugo hiyo kufa ,kwa sababu ugonjwa unakuta tayari miili ya mifugo hiyo imedhoofika sana. Katika hili Dkt Sigala amewashauri wafugaji kuwa na maeneo ya malisho, ambayo watakuwa wanapanda nyasi, na hatimaye  kuweza kuyatumia  maeneo hayo kulisha mifugo yao wakati wa ukame. Dkt. Sigala amesema kwamba wanaendelea kutoa elimu hiyo ya upandaji nyasi za kulishia mifugo ,na tayari wameshaleta mbegu,na baadhi ya wafugaji wameshaanza kuja kuchukua mbegu hizo na kwenda kupanda.Vilevile amesema kwamba wale wafugaji wenye mifugo mingi ni vema wakajenga majosho yao wenyewe na wakajiwekea utaratibu mzuri wakuogesha mifugo yao, kwani wapo wafugaji ambao kwa idadi ya mifugo waliyonayo wana uwezo wa kujenga majosho yao .Sambamba na hayo Dkt. Sigala amewataka wafugaji kuacha imani potofu kwamba wakati wa kiangazi hakuna kupe, hivyo kuona kwamba hawana sababu ya kuogesha mifugo wala kuipatia kinga katika kipindi hicho, jambo ambalo ndio kiini hasa cha mashambulizi ya ugonjwa  wa kupe  unaoua mifugo  wakati huu .

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa