Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto imeazimia kuandaa Wiki ya Kilimo na Ufugaji kabla ya kuanza kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2025/2026, ikiwa ni hatua ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kuongeza tija katika sekta za kilimo na ufugaji.
Dhamira hiyo imewekwa wazi na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhe. Remidius Mwema, alipokuwa akizungumza Agosti 6, 2025 alipotembelea banda la Kiteto katika maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kwenye viwanja vya Themi Njiro, mkoani Arusha, ambapo alikuwa mgeni rasmi wa siku hiyo.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mhe. Mwema aliagiza wataalamu wa sekta ya kilimo na mifugo kutoka Kiteto ambao wamefika kwenye maonesho hayo, kuhakikisha wanatembelea mabanda ya wadau wa kilimo na mifugo yaliyopo kwenye maonesho hayo ili kueleza dhamira hiyo na kuanzisha mahusiano na mtandao wa ushirikiano kwa ajili ya maandalizi ya tukio hilo muhimu.
Mkuu huyo wa wilaya pia alitumia fursa hiyo kuwashirikisha moja kwa moja wadau aliowatembelea kwenye mabanda yao, ambao walipokea kwa furaha mpango huo na kuahidi kushiriki kikamilifu. Baadhi ya wadau hao walienda mbali zaidi kwa kujitolea kudhamini shughuli hiyo inayolenga kuongeza maarifa, ubunifu na tija kwa wakulima na wafugaji wa Kiteto.
Wiki ya Kilimo na Ufugaji inatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kutoa elimu, kuonesha teknolojia mpya, pamoja na kuwajengea uwezo wakulima na wafugaji ili kuongeza uzalishaji na kipato.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa