Walengwa wa TASAF katika vijiji vya Dongo na Olgila wilayani Kiteto wakiwa katika zoezi la uhawilishaji fedha na uhakiki wa watoto wanaopaswa kuwepo kwenye huduma za afya na elimu zinazotolewa na TASAF kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN)
Walengwa wa TASAF katika vijiji vya Dongo na Olgila wilayani Kiteto wakipokea fedha ya ruzuku inayotolewa na TASAF kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN)
Mlengwa wa TASAF katika kijiji cha Dongo wilayani Kiteto Rahel Wiliam Christopher aliyefanikiwa kuboresha maisha yake kutokana na ruzuku inayotolewa na TASAF kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN).
Nguruwe wa mlengwa wa TASAF katika kijiji cha Dongo Wilayani Kiteto Rahel Wiliam Christopher. Nguruwe hawa wamenunulia kwa fedha ya ruzuku inayotolewa na TASAF kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN)
Nyumba ya Mlengwa wa TASAF katika kijiji cha Dongo wilayani Kiteto Rahel Wiliam Christopher.Nyumba hii imejengwa kwa fedha ya ruzuku inayotolewa na TASAF kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN)
Mlengwa wa TASAF katika kijiji cha Olgila wilayani Kiteto Katarina Elias aliyefanikiwa kuboresha maisha yake kutokana na fedha ya ruzuku inayotolewa na TASAF kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN).
Mbuzi wa mlengwa wa TASAF katika kijiji cha Olgila Wilayani Kiteto Katarina Elias. Mbuzi hawa wamenunuliwa kwa fedha ya ruzuku inayotolewa na TASAF kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN)
Nyumba aliyokuwa akiishi mlengwa wa TASAF katika kijiji cha Olgila wilayani Kiteto Katarina Elias kabla ya kuanza kupata ruzuku inayotolewa na TASAF kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN)
Nyumba ya Mlengwa wa TASAF katika kijiji cha Olgila wilayani Kiteto Katarina Elias.Nyumba hii imejengwa kwa fedha ya ruzuku inayotolewa na TASAF kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN)
Mlengwa wa TASAF katika kijiji cha Olgila wilayani Kiteto Penina Kilongola Magoha aliyefanikiwa kuboresha makazi yake kutokana na fedha ya ruzuku inayotolewa na TASAF kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN)
Nyumba ya Mlengwa wa TASAF katika kijiji cha Olgila wilayani Kiteto Penina Kilongola Magoha.Nyumba hii imejengwa kwa fedha ya ruzuku inayotolewa na TASAF kupitia Mpango wa kunusuru Kaya Maskini (PSSN)
Mlengwa wa TASAF katika kijiji cha Olgila wilayani Kiteto Esta Bilishani Mkali aliyefanikiwa kuboresha maisha yake kutokana na ruzuku inayotolewa na TASAF kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN).
HABARI KAMILI....
WALENGWA WA TASAF WILAYANI KITETO WAKIRI KUBORESHEWA MAISHA NA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI (PSSN)
Walengwa wa TASAF wilayani Kiteto wamesema kwamba Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN) umewaboreshea maisha .Walengwa hao wameyasema hayo wakati wa zoezi la uhawilishaji fedha awamu ya tatu, dirisha la malipo la mwezi Novemba - Decemba na uhakiki wa watoto wanaopaswa kuwepo kwenye huduma za afya na elimu .
Akizungumza baada ya kupokea fedha za ruzuku, mlengwa wa TASAF katika kijiji cha Dongo Rahel Wiliam Christopher amesema kwamba PSSN imeboresha maisha yake, kwani kwa kutumia fedha za TASAF ameweza kununua Nguruwe na kuku ambao anawafuga, anapowauza anapata fedha ,ambazo anazitumia kukidhi mahitaji ya lazima ya familia yake. Pia ameweza kujenga nyumba ya vyumba viwili ambayo iko kwenye lenta. Rahel anasema‘‘tangu nimeanza kupokea hela za TASAF sihangaiki sana.kama nimeishiwa sabuni naweza nikachukua kuku wangu mmoja nikauza , pia kupitia hela hiyo hiyo ya TASAF napata mahitaji ya watoto kama sare za shule na madaftari .
Mlengwa wa TASAF Esta Bilishani Mkali amesema kwamba PSSN imeboresha maisha yake,kwani kabla hajaingia kwenye PSSN hakuwa na chochote , Esta anasema ‘‘TASAF imeboresha familia yangu , kwa kutumia fedha za TASAF nimeweza kununua mbuzi watatu,kuku nane ,pia imenisaidia kupata matibabu ya mtoto. Mtoto wangu alikuwa anasumbuliwa sana na macho, lakini sikuwa na fedha ya kumpeleka hospitali, baada ya kuanza kupokea fedha za TASAF, niliweza kukusanya kidogo kidogo hadi nikafanikiwa kumpeleka mtoto wangu hospitali Morogoro kupata matibabu’’. Aidha Esta amesema kwamba lengo lake ni kununua ng’ombe wa maziwa, hivyo mbuzi alionao watakapo ongezeka atawauza , pia fedha anayopewa na TASAF atakuwa akiweka kidogo kidogo ili aweze kutimiza lengo hilo.
Vilevile mlengwa wa TASAF Katarina Elias amesema kwamba PSSN imeboresha maisha yake .Katarina anasema ‘‘ Nilikuwa nateseka sana, kwenye miraba kila siku kulima vibarua ili niweze kuishi, lakini TASAF imenisaidia, kabla sijaingia kwenye mpango wa TASAF nilikuwa naishi kwenye nyumba ya nyasi, nimeweza kujenga nyumba nyingine ambapo kwa kutumia hela ya TASAF nilinunua bati saba nikapaua nyumba yangu , nimenunua mbuzi nane, na ninapata fedha ya kujikimu kwa mahitaji yangu madogo madogo ya nyumbani’’.
Kadhalika mlengwa mwingine wa TASAF Penina Kilongola Magoha amesema kwamba PSSN imeboresha maisha yake kwani kwa kutumia fedha za TASAF ameweza kupaua nyumba yake kwa bati, na pia inamsaidia kupata mahitaji yake madogo madogo ya kila siku,tofauti na wakati kabla hajaingia kwenye PSSN ambapo hali yake ya maisha ilikuwa ngumu na alikuwa na makazi duni.
Katika hatua nyingine Afisa ufuatiliaji wa TASAF wilaya ya Kiteto ndugu Kishari Shegela amewataka walengwa wa TASAF katika kijiji cha Olgila kuhakikisha kwamba wanakamilisha michango yao ya Bima ya afya (ICHF) mara tu wanapopokea ruzuku zao ili kupata kadi za bima ya afya ambazo zitawawezesha kupata matibabu pindi watakapougua.Shegela anasema ‘‘bima ya afya itakusaidia, ukilazwa hospitali hata siku saba tu,unaweza kutumia pesa zaidi ya shilingi 50,000, lakini bima ya afya unailipia shilingi 30,000 tu na unatibiwa wewe, mwenzi wako na watoto wako kwa mwaka mzima.
Aidha ndugu Shegela amewataka walengwa wa TASAF kuzitumia vizuri fedha wanazopewa na TASAF. Akisisitiza kuhusu matumizi bora ya fedha hizo Shegela anasema ‘‘Jamani hizi fedha sio za kula tu, tafuta kitu uwekeze,tafuta kabiashara,sio kila fedha unayopata unakula tu , jiunge kwenye kikundi, peleka kidogo kwenye VICOBA, cheza hata kamchezo katakusaidia kupata sare za shule na mahitaji mengine ya familia’’Shegela anaendelea kusema kwamba walengwa wa TASAF waandikishe kwenye mpango watoto wote walio katika kaya zao ambao wanasoma shule na wale ambao wanahudhuria kliniki, na wahakikishe kwamba watoto wanaotakiwa kuhudhuria kliniki wanapelekwa kliniki kwani kutowaandikisha, na kutowapeleka kliniki kunasababisha kutokupata ruzuku zao.Pia amewataka walengwa hao kununua mahitaji muhimu ya watoto wao,kama, sare za shule, masweta na viatu vya shule, kwani ,katika ruzuku wanazopewa , kuna ruzuku ya elimu ambayo walengwa ni hao watoto, hivyo wazazi ama walezi wanapopokea fedha hizo wafahamu kwamba wanapaswa kuwanunulia watoto wao mahitaji yao ya shule na si kwamba wazitumie zote.
Katika wilaya ya Kiteto, TASAF kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN) ina walengwa 5739, ambapo idadi hiyo inajumuisha walengwa wanaopatiwa ruzuku ya msingi na ruzuku ya masharti ambayo hutolewa kwa walengwa wenye watoto wanaohudhuria kliniki na watoto wanaosoma elimu ya msingi na sekondari kidato cha kwanza hadi kidato cha sita.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa