Wizara ya Afya(Mpango wa Taifa wa Afya na Lishe Shuleni na Mpango wa Taifa wa Chanjo) Juni 5 ,2025 imeendesha mafunzo kwa walimu wa shule za msingi na sekondari kuhusu afua jumuishi za elimu ya afya shuleni.
Mafunzo hayo ambayo yalifanyika katika kanda tatu (Kibaya, Sunya na Engusero), yalilenga kutoa elimu kuhusu magoniwa yanayozuilika kwa chanjo ikiwemo chanjo ya kuzuia Saratani ya Mlango wa Kizazi(HPV), lishe, afya ya uzazi kwa vijana balehe, usafi wa mazingira na umuhimu wa uanzishwaji wa Klabu za Afya shuleni.
Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Chanjo kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI, na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wadau mbalimbali katika utekezaji wa Afua za Elimu ya Afya na chanjo shuleni imeandaa kampeni ya kuhamasisha chanjo ya kuzuia Saratani ya Mlango wa Kizazi(HPV) katika Halmashauri mbili za Babati Mji na Kiteto mkoani Manyara.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa