Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), kupitia Mradi wa BOOST, inaendesha mafunzo maalumu ya siku nne kwa Walimu wa Darasa la Awali na Walimu Wakuu kutoka shule 46 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto. Mafunzo hayo yameanza tarehe 9 Januari 2025 katika Ukumbi wa Maktaba.
Mafunzo haya ni sehemu ya afua za Mradi wa BOOST, ambayo inalenga kuboresha utoaji wa mafunzo endelevu kazini kwa walimu (MEWAKA). Lengo kuu ni kuwapatia walimu ujuzi katika ufundishaji wa watoto wa awali, kwa kutumia mbinu bora, miongozo, na jinsi ya kutengeneza zana za kufundishia.
Kwa mujibu wa Mwalimu Elizabeth Mlaponi, Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi, mafunzo hayo yamehudhuriwa na jumla ya walimu 92 kutoka shule hizo 46. Ameeleza kuwa mafunzo haya yanafanyika kwa awamu, hivyo walimu wa shule nyingine walishapokea mafunzo kabla ya awamu hii.
Aidha Mwl. Mlaponi amesema kwamba mafunzo hayo yanatarajiwa kuleta maboresho makubwa katika sekta ya elimu kwa maana mtoto anatakiwa kuandaliwa mapema kwa kumjengea msingi imara katika ujifunzaji hivyo kuleta ufanisi kitaaluma katika sekta ya elimu.
"Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuleta maboresho makubwa katika sekta ya elimu", ameongeza Mwl. Mlaponi.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa