• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

"Wanafunzi Wote Wawepo Darasani Ifikapo Januari 15,2024."-DC Mwema

Imetumwa : January 8th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mh.Remedius Mwema Emmanuael ameagiza ifikapo Januari 15, 2024, wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza na watoto  wote waliofikia umri wa kuanza darasa la awali na darasa la kwanza,  wawe wameshawasili shuleni kuanza masomo.

Mwema ameyaongea hayo Januari 8, 2023 wilayani Kiteto kwenye ziara ya  kukagua na kuhakiki idadi ya wanafunzi wa awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza walioripoti shuleni.

Mh Mwema alisema kwamba serikali imebeba gharama za ada kwa wanafunzi wote hivyo hakuna sababu inayofanya mwanafunzi asiwepo darasani. “Na tulishatoa maelekezo kua hata kama mwanafunzi hana sare za shule au madaftari apokelewe wakati mzazi anaendelea kujipanga kukamilisha hayo mahitaji”’ aliongeza Mh. Mwema.

Aidha Mh Mwema alitoa maagizo kwa Maafisa Elimu Kata na watendaji wote wa vijiji na kata kuingia mitaani nyumba kwa nyumba kuhakikisha  watoto wote waliofikia umri wa kuanza darasa la awali na la kwanza wamendikishwa na wanaenda shule na wale waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wote nao wameripoti shuleni. 

“Upande wa wale waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza, nahitaji orodha ya wote ambao hawajaripoti shuleni na kila mtoto nipewe sababu kwanini hayupo darasani nahitaji na namba ya simu ya mzazi au mlezi”, alisema Mwema.

Vilevile, Mh Mwema alimuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilayani Kiteto, kuanza kukamata wazazi/walezi ambao watoto wao watakua hawajaripoti shuleni kuanzia Januari 15, 2024.

Mbali na kuweka juhudi kwa wanafunzi hao wapya, Mh Mwema pia aliagiza kwamba wanafunzi wanaoendelea nao wafuatiliwe kama wote wamerudi shuleni ili kuthibiti wanafunzi kuacha shule.

Katika ziara hiyo ambayo Mkuu wa Wilaya aliambatana na wataalamu mbalimbali wa halmashauri pamoja na Kaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi Kiteto, alikagua shule nne za msingi ambazo ni Boma, Kibaya, Chemchem  na Kijungu. Upande wa shule za sekondari ni Kiteto na Kibaya.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa