Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mh. Remidius Mwema, ameagiza kila mwananchi wa kata ya Matui na Bwawani kupanda miti miwili katika msimu ujao wa mvua.
Maagizo hayo ameyatoa Mei 20, 2024 katika ziara alizofanya katika kata hizo. Lengo la ziara ilikua kujitambulisha na kusikiliza kero za wananchi katika kata hizo.
Aidha Mh. Mwema amewashauri wananchi wa kata hizo kupanda miwa pembezoni mwa makorongo ili kuzuia kuongezeka kwa mmomonyoko katika maeneo hayo. Upandaji wa miwa utawasaidia pia wananchi hao kuwaongezea kipato.
Mbali na hayo, katika ziara hizo, Mh. Mwema alikemea vitendo vya rushwa wa kuwaasa watumishi na wananchi kutotoa wala kupokea rushwa. Aidha alilisitiza wananchi wasije kulaghaiwa na mtu yoyote kwamba wachange fesha ili kwenda kumuona maana yeye ni Mkuu wa Wilaya wa watu wote hivyo kumuona yeye haihitaji kutoa pesa yoyote.
Kuhusu migogoro mbalimbali wilayani hapo, Mh. Mwema amesema amedhamiria kuhakikisha sifa ya migogoro wilayani hapo inaisha. Aidha amesema kwamba yeye pamoja timu yake watapita kwenye nyanda zote za malisho ili kutatua migogoro katika nyanda hizo. Hata hivyo ametoa wito kwamba kama kuna mtu amevamia nyanda ni vyema akaondoka yeye mwenyewe ila endapo kuna mkulima amekutwa na nyanda, atapewa haki yake.
Vilevile katika kata zote mbili, Mh. Mwema amewaambia wananchi juu ya umuhimu wanafunzi kula chakula shuleni na kusema kwamba suala la chakula shuleni ni ajenda ya kitaifa.
Mbali na hayo, Mh. Mwema ameonya wafugaji wanaopitisha mifugo kwenye kwenye barabara na kuwaagiza watendaji kuwachukulia hatua wote wanaopitisha mifugo kwenye barabara. Halikadhalika, aliwaonya wakulima wanaolima mpaka kwenye hifadhi za barabara na kuagiza kuanzia msimu ujao wote watakaolima mpaka kwenye hifadhi za barabara watachukuliwa hatua.
https://www.instagram.com/p/C7OXn6wotqW/?igsh=MWpzenhrcmJ4azJyZg==
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa