Jumla ya Wasimamizi Wasaidizi 46 wa Uchaguzi Mkuu ngazi ya kata wameanza mafunzo rasmi kujiandaa na zoezi la Uchaguzi Mkuu 2025.
Mafunzo hayo ya siku mbili yalianza rasmi jana Agosti 4,2025 na yanatarajiwa kukamilika ifikapo Agosti 6, 2025. Kabla ya kuanza mafunzo, wasimamizi hao walikula viapo viwili muhimu mbele ya Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Kibaya-Kiteto Mhe. Aron Erasto Losioki, kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa pamoja na kiapo cha kutunza siri, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha uadilifu na kutokuwa na upendeleo katika kipindi cha uchaguzi.
Zoezi la mafunzo hayo linaendeshwa kwa mujibu wa miongozo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), kwa lengo la kuhakikisha wasimamizi wote wanakuwa na uelewa wa kina juu ya taratibu, sheria, na kanuni za uchaguzi.
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unatarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025, na kauli mbiu ni Kura yako Haki yako Jitokeze Kupiga Kura.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa