Wataalamu kutoka Kituo cha Ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma (PPP Centre), Aprili 9, 2025, wametoa elimu kwa Wakuu wa Idara na Vitengo wilayani Kiteto.
Elimu hiyo ya Ubia imelenga kufanikisha uibuaji wa miradi inayoweza kutekelezwa kwa utaratibu wa Ubia (Public Private Partnership).
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kiteto, CPA. Hawa Abdul Hassan,aliwakaribisha wataalamu hao na kuwasihi Wakuu wa Idara na Vitengo kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo ili yaweze kuleta chachu ya maendeleo kwa wananchi na wakazi wa Halmashauri ya Kiteto, Mkoa wa Manyara, na Taifa kwa ujumla.
Mafunzo haya ambayo yaliendeshwa na Dr. Kafigi Jeje akishirikiana na Ndg. Brian Dancan, yalijikita kwenye kujenga uwezo wa halmashauri katika uibuaji na usimamizi wa miradi inayoendeshwa kwa utaratibu wa Ubia.
Mkurugenzi Mtendaji, aliwashukuru kwa mafunzo hayo na kuahidi kushirikiana na Kituo cha ubia ili malengo ya mafunzo hayo yafikiwe haraka.
Vile vile, baada ya mafunzo hayo, wageni hao walipata fursa ya kufanya kikao kifupi na wataalamu mbalimbali wa Halmashauri na baadaye kutembelea maeneo mbalimbali ili kufanya tathimini ya maeneo ambayo miradi ya maendeleo inaweza kuibuliwa.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa