Mwenyekiti wa Kikao cha DCC Mhe. Tumaini Magessa akizungumza wakati wa Kikao cha DCC kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto.
Wajumbe wa Kikao cha DCC wakiwa katika Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto.
Wajumbe wa Kikao cha DCC wakishauri juu ya masuala mbalimbali yanayohusu wilaya ya Kiteto wakati wa Kikao cha DCC kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania usharika wa Kibaya akifanya sala baada ya mwenyekiti kufunga kikao cha DCC kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
....................HABARI KAMILI......................
"Watendaji wa Vijiji Tekelezeni Majukumu Yenu Migogoro Isiendelee kuichafua Wilaya ya Kiteto ’’ DC Magessa
Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mheshimiwa Tumaini Magessa amewataka watendaji wa vijiji wilayani Kiteto kutekeleza majukumu yao ili kumaliza migogoro inayotokea katika vijiji vyao .Mhe. Magessa ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ( DCC) kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
Mheshimiwa Magessa amesema kwamba migogoro yote inayoendelea wilayani Kiteto inawezekana kwisha kabla ya kufika ofisini kwake ikiwa watendaji wa vijiji watafanya kazi zao kama inavyotakiwa, kwa sababu wao ndio wanaoishi na wananchi ,wanatakiwa kuigundua migogoro inayotokea katika vijiji vyao na kuishughulikia ili kuitatua .Akitoa maelekezo kwa watendaji wa vijiji kuhusu namna ya kushughulikia migogoro hiyo Mhe. Magessa anasema ‘‘kila mtendaji awe na rejista ya migogoro, inayoonyesha migogoro yote , na nini kijiji kimefanya juu ya migogoro hiyo. Atuambie mimi nimetatua moja, mbili , nimeshindwa hapa.Tunapata shida sana kwa sababu huko katika ngazi ya vijiji watu hawafanyi kazi ,mambo ya uongo yanafika huku DC ndiye ninayekuja kuyagundua.Watu wanakuja na migogoro na uongo mwingi.Ukisinzia kidogo uongo huo unapita’’.
Aidha Mhe. Magessa amesema kwamba kuna kazi kubwa sana ya kufanya ili mambo yaende na yaishie katika ngazi za vijiji.Kazi hiyo ni kuwafanya watendaji wawajibike ipasavyo. Akisisitiza kuhusu uwajibikaji kwa watendaji wa vijiji,Mhe. Magessa anasema “Watendaji wa vijiji fanyeni kazi, migogoro ikifika katika ofisi zenu za vijiji, ishughulikiwe hapo, iishe isiendelee kuichafua wilaya yetu”. Kadhalika Mhe. Magessa amesema kwamba watendaji wakifanya kazi, migogoro mingi itashughulikiwa katika ngazi za vijiji na vitongoji na ikifika katika ngazi ya wilaya ,utatuzi wake utakuwa umekamilika. Na kwamba ni kwa namna hiyo tu ndio watafanikiwa kumaliza migogoro wilayani Kiteto.
.................... MWISHO ......................
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa