Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mh. Remidius Mwema Emmanuel, awaasa watumishi wa Halmashauri, taasisi za serikali na binafsi kua na nidhamu nzuri ya kazi na kufanya kazi kwa uadilifu.
Hayo ameyaongea Januari 11, 2024 katika Ukumbi wa Maktaba wilayani hapo kwenye kikao cha kujitambulisha kwa watumishi hao wa Halmashauri na taasisi mbalimbali zilizopo wilayani hapo.
Mbali na hayo Mh. Mwema aliwasisitiza watumishi hao kuheshimiana na pia kutoa huduma bora kwa kila mtu na kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo inayowapasa na pasipo kupendelea kundi fulani. “Nawaomba sana tumuhudumie mtu kwa utu wake na sio kwa kuangalia sura wala muonekano wake”, alisisitiza Mh. Mwema.
Awali Mkuu huyo wa Wilaya alisema kwamba siku chache baada ya kuwasili Kiteto alienda katika Hospitali ya wilaya kupata huduma ya matibabu pasipo kujitambulisha wadhifa wake na alipewa huduma nzuri. Kutokana na hilo, Mh. Mwema alimpongeza Mganga Mkuu wa Wilaya pamoja na watumishi wote wa Hospitali hiyo kwa huduma bora wanayotoa kwa wananchi.
Mbali na hayo, Mkuu huyo wa Wilaya alisema kwamba yupo tayari kupokea ushauri na maoni kutoka kwa wafanyakazi hao. “Kua kiongozi haimaanishi kua unajua kila kitu, nipo tayari kujifunza na kupokea ushauri na maoni kutoka kwenu”, aliongeza Mh. Mwema.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa