• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Watumishi wa Serikali Kataeni Kutumiwa na Wanasiasa - RC Mnyeti

Imetumwa : January 9th, 2018


                    Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti akizungumza na watumishi wa serikali,wenyeviti wa vijiji na Wahe. madiwani  katika kikao chake kilichofanyika ndani ya ukumbi  wa kituo cha jamii ( Community Center) Kibaya - Kiteto

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa  Akimkaribisha  Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti  Katika  Kikao cha Mhe.  Mkuu wa Mkoa na Watumishi wa Serikali,Wenyeviti wa Vijiji Pamoja na Wahe. Madiwani .


Watumishi wa Serikali,Wenyeviti wa Vijiji  pamoja na Wahe. Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti  ndani ya Ukumbi wa Kituo cha Jamii ( Community Center) Kibaya - Kiteto.

 

                                                                                                    ......... HABARI KAMILI...........



WATUMISHI WA SERIKALI KATAENI KUTUMIWA NA WANASIASA- RC MNYETI.

Mkuu wa mkoa wa Manyara mheshimiwa Alexander Mnyeti amewataka watumishi kukataa kutumiwa na wanasiasa kukwamisha shughuli za serikali na kuchochea migogoro.Mheshimiwa Mnyeti ameyasema hayo katika kikao chake na watumishi wa serikali,wenyeviti wa vijiji pamoja na waheshimiwa madiwani  kilichofanyika ndani ya ukumbi wa Kituo cha jamii (Community Center ) kilichopo katika mji mdogo wa Kibaya wilayani Kiteto.

Akizungumza katika kikao hicho mheshimiwa  Mnyeti amesema kwamba kuna wanasiasa ambao  wanaikwamisha serikali kufanya shughuli zake  , na wamekuwa wakiwatumia watumishi wa serikali katika kufanya hivyo kwa kuwatishia kuwafukuza kazi pale wanapokuwa hawakubaliani na matakwa yao . Aidha Mheshimiwa Mnyeti amesema kwamba watumishi  wachape kazi , wafanye kazi  kulingana na taaluma zao, wawe na misimamo katika yale wanayoamini kwamba ni sahihi , wasimame katika kutenda haki ,wasiyumbishwe wala kutikiswa na wanasiasa .Akisisitiza kuhusu kuwa na msimamo katika kufanya kazi, mheshimiwa Mnyeti anasema ‘‘ Watendaji wa vijiji,watendaji kata, wakuu wa idara ,kataeni kwa nguvu moja msiwe sehemu ya kutumika ,msitumiwe na wanasiasa  kwa sababu zao binafsi,na kwa faida zao binafsi.Nitasikitika sana kuona mambo hayaendi ,eti kwa sababu kuna mwanasiasa anazuia. Kila mtu atimize wajibu wake. Mtendaji wa kata utakaekuja kuniambia kwamba  umesimamishwa kazi kwa sababu  umekataa maelekezo ya mbunge nitakuelewa na nitakutafutia cheo kingine’’.

Vilevile mheshimiwa Mnyeti amezungumzia suala la nidhamu kwa watumishi wa serikali ambapo  amesema kwamba watumishi wengi wamesahau wajibu wao, wanajua muda wanaotakiwa kufika kazini na muda wa kutoka kazini, lakini wanaingia kazini kwa muda wanaotaka, na wanatoka kwa muda wanaotaka .Akisisitiza kuhusu kuwawajibisha watumishi wasiofuata maadili ya utumishi, mheshimiwa  Mnyeti  anasema ‘‘Tuna staili nyingi za kumfukuza mtu kazi ,na wala hatutishii, tukiona hii staili ya madiwani imeshindikana tuna staili nyingine.Ama tutakuwa tunawahamishia maeneo mengine ambayo wako tayari kuwajibisha watumishi wao’’. Kadhalika amewataka watumishi kuacha siasa maofisini , badala yake wafanye kazi zao.

Katika kikao hicho pia Mheshimiwa Mnyeti  amezungumzia mambo mbalimbali ikiwemo  makusanyo ya kodi  ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wilaya ya Kiteto ambapo amesema kwamba mapato yako chini ,hivyo amemuagiza Mkurugenzi  mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Tamim Kambona kwa kushirikiana na afisa biashara  kumpa meneja wa TRA Wilaya ya Kiteto orodha ya wafanyabiashara wote ili aweze kuchambua wafanya biashara wanaopaswa  kulipa kodi TRA , baada ya uchambuzi huo watendaji wa kata na vijiji wamsaidie kumuonyesha maeneo waliko wafanyabiashara hao.Kadhalika  mkuu  wa wilaya  mheshimiwa Tumaini Magessa  ambaye ndiye mshauri wa kodi wa wilaya ameagizwa  kuitisha mikutano ya mara kwa mara  ili kuhakikisha  kwamba maelekezo aliyoyatoa mkuu wa mkoa  yanafanyiwa kazi , lengo likiwa ni kuongeza mapato .Pia amezungumzia kuhusu viongozi na watumishi  kufanya biashara na halmashauri ambapo amesisitiza kwamba hairuhusiwi kisheria, na ni marufuku kufanya hivyo.

Katika hatua nyingine mheshimiwa Mnyeti amezungumzia kuhusu ukataji miti, katika hilo  ametoa utaratibu wa kukata miti ambapo  ni mti mmoja kwa miti kumi , kwamba   mtu haruhusiwi kukata mti hata mmoja isipokuwa amepanda miti kumi na imeshika  vizuri ardhini .Pia ameelekeza utaratibu wa kufuata  ili kupata kibali cha kukata miti baada ya kupanda miti hiyo kulingana na idadi ya miti mtu anayotaka kukata . Pia amezungumzia matumizi bora ya ardhi ambapo amemtaka mkuu wa wilaya kusimamia matumizi ya ardhi kulingana na sheria na taratibu ambazo zilikwisha kubalika. Sambamba na hayo, mheshimiwa  Mnyeti amezungumzia suala la chakula cha mchana  mashuleni ,ambapo ametoa agizo kwamba wanafunzi wapate chakula cha mchana , na wanaokwamisha utaratibu huo wachukuliwe hatua.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa