Watumishi wilayani Kiteto wameaswa kua na nidhamu na matumizi bora ya fedha ikiwa ni njia mojawapo ya kupata utulivu kazini.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya Kiteto , Mh. Remidius Mwema, kwenye Madhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo wilayani hapo yamefanyika Aprili 29,2024.
Mh. Mwema amewaasa watumishi kujiepeusha na mikopo isiyo na lazma na kuepeuka mikopo kutoka kwenye taasisi zisizo rasmi.
“Lazma kuwe na nidhamu na matumizi bora ya fedha, epukeni mikopo isiyo ya lazma. Mtumishi kama hayupo imara kiuchumi na mikopo kila mahali hawezi kupata utulivu wa akili na kufanya kazi kwa ufanisi” ameongeza Mh. Mwema.
Mh. Mwema pia amewashauri watumishi hao kujishughulisha na ujasiriamali ili kujiongezea kipato.
Mbali na hayo, Mh. Mwema amewasihi watumishi hao kutoa huduma bora kwa watu wote pasipo kuangalia muonekano wa mtu.
“Unaweza kuondoa baraka za Mungu katika maisha yako kwa kuwahudumia watu vibaya” ameongeza Mh. Mwema.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya amewaasa watumishi hao kua makini na mitandao ya kijamii kwa kuwataka kulinda utu wao.
Kauli Mbiu katika ya Mei Mosi 2024 “Nyongeza ya Mshahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha”
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa