Oktoba 30,2023, Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto imeadhimisha Siku ya Lishe Kitaifa katika Shule ya Sekondari Kibaya.
Katika maadhimisho hayo, Afisa Lishe (W), Bi Beatrice Lutanjuka akiongozana na wataalam wengine wa lishe kutoka katika ofisi yake, walitoa elimu kuhusu ulaji wa mlo kamili kwa vijana rika balehe shuleni hapo.
Vilevile katika maadhimisho hayo, Bi Lutanjuka alitumia jukwaa hilo kuhamasisha utekelezaji wa afua ya utoaji wa chakula na lishe shuleni kwa kueleza faida za utoaji wa chakula na lishe shuleni.
“Zipo faida nyingi za ulaji wa chakula shuleni ikiwemo kuongeza ufaulu, kuongeza mahudhurio na pia hata kujenga umoja kati yenu hivyo niwaombe muwafikishie wazazi wenu ujumbe kuhusu kutekeleza agizo la kuleta chakula shuleni ili wote muweze kupata chakula shuleni na kwasasa kula shuleni sio hiyari bali ni lazma” aliongeza Bi. Lutanjuka.
Mbali na hayo, katika maadhimisho hayo Bi Lutanjuka pamoja na timu yake walikagua bustani ya mboga shuleni hapo na kutoa ushauri kwa uongozi wa shule kuongeza bustani ya matunda maana kwa sasa shule hiyo ina bustani ya mbogamboga tu.
Hali kadhalika, wataalam hao wa lishe walifanya tathmini ya hali ya lishe kwa vijana balehe 114. Katika tathmini hiyo 15 % ya vijana hao walibainika kua na uzito pungufu, 9% walionekana kua na uzito uliozidi na 2% ya vijana hao walibaika kua na uzito mkubwa zaidi. Kutokana matokeo hayo wataalam hao walitoa ushauri nahisi kuhusiana na lishe kwa kijana mmoja mmoja ambao katika tathimini hiyo walibainika kua uzito pungufu, uzito uliozidi na uzito mkubwa zaidi.
Kitaifa maadhisho ya Siku ya Lishe yamefanyika Mkoa wa Pwani Oktoba 30, 2023 na kauli mbiu ya mwaka huu ni; “Lishe Bora kwa Vijana Balehe, Chachu ya Mafanikio Yao”.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa