• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Ziara ya Mbunge Papian, Matumaini mapya kwa Wana Ngabolo

Imetumwa : July 9th, 2018

Mbunge wa Kiteto Mhe. Emmanuel Papian akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ngabolo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini Ngabolo mwishoni  mwa wiki.


Mtendaji wa Kijiji cha Ngabolo akitambulisha  uongozi wa serikali ya Kijiji  chake  katika Mkutano wa hadhara uliofanyika  kijijini  Ngabolo mwishoni mwa wiki.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngabolo akifungua Mkutano wa hadhara uliofanyika katika  kijiji hicho mwishoni mwa wiki.

Wakazi wa kijiji cha Ngabolo wakiwa wamekusanyika  kumsikiliza Mbunge wao Mhe. Emanuel Papian katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijijini Ngabolo mwishoni mwa wiki.


Wakazi wa kijiji cha Ngabolo wakimuuliza maswali Mbunge wao Mhe. Emanuel Papian katika mkutano wa hadhara uliofanyika  kijijini Ngabolo mwishoni mwa wiki.

Mbunge wa Kiteto Mhe. Emmanuel Papia pamoja na ujumbe wake kutoka wilayani wakikagua  madarasa yaliyojengwa kwa ajili ya shule ya msingi  katika Kijiji cha Ngabolo ambayo ujenzi wake unaendelea . Madarasa hayo manne yamejengwa kwa nguvu za wananchi , na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Ndg Tamim Kambona ametoa mabati ambayo ndiyo yaliyopaulia madarasa hayo . 


Msingi huu ni wa jengo la madarasa matatu ambayo yanajengwa kwa nguvu za wananchi ili kukamilisha madarasa saba kwa ajili ya shule ya msingi  katika Kijiji cha Ngabolo  .


Mbunge wa Kiteto Mhe. Emmanuel Papia pamoja na ujumbe wake kutoka wilayani wakikagua ujenzi wa nyumba ya mwalimu  kwa ajili ya shule ya msingi  katika Kijiji cha Ngabolo ambayo ujenzi wake unaendelea .




......HABARI KAMILI.......



Ziara ya Mbunge wa Kiteto Mhe. Emmanuel Papian  imeleta matumaini mapya kwa wanakijiji wa Ngabolo,ambapo Mbunge huyo amewahakikishia kukamilika kwa usajili wa shule ya msingi na uletwaji wa walimu katika shule hiyo ambayo wameijenga kwa nguvu zao, sambamba na kutengeneza mashine iliyokuwa ikitumika kupandisha maji katika kijiji hicho,ambayo imeharibika.Mhe Papian ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini Ngabolo mwishoni mwa wiki.


Akizungumza katika mkutano huo Mheshimiwa Papian amesema” Nimeona mmejenga madarasa manne, na mengine matatu yako kwenye msingi, nimeona na tofali ambazo mmefyatua kwa ajili ya kupandisha yale madarasa matatu ambayo yako kwenye msingi. Diwani wenu amenihakikishia kwamba madarasa yale matatu ambayo yako kwenye msingi yatakamilika ndani ya muda mfupi.Suala hili naondoka nalo,nitalifuatilia kwa nguvu zangu zote mpaka shule ifunguliwe.Tumekubaliana, na mwenyekiti wa chama ,tumekubaliana na katibu, tumekubaliana na diwani wenu hapa ,tunakwenda kukutana na wahusika tujadiliane, tupange, tukubaliane, shule isajiliwe , ifunguliwe, Januari watoto waanze kusoma hapa . Hatutaki siasa tena,tunataka hii  ifunguliwe.watoto wetu wasomee hapa, walioko Ndedo wasogee hapa, tupunguze msongamano kwenye shule ya Ndedo.


Kadhalika Mhe. Papian amezungumzia kuhusu maji,ambapo maji imekuwa ni tatizo kubwa sana kwa wakazi wa Ngabolo, hususani baada ya bwawa la kijiji hicho kupasuka  na mashine ya maji kuharibika. Hapa Mhe Papian amesema “ Nimeuliza hapa kuhusu mashine ya maji,nimeambiwa mashine inasumbua.Ni lazima tupate mpango mahususi, ambao unaoeleweka,kuhakikisha kwamba huduma ya maji ya uhakika inapatikana hapa Ngabolo.Nitazungumza na mzabuni ambaye yupo tujue ni nini ambacho kinatakiwa kifanyike ili mashine iendelee kuzalisha maji kwa ajili ya binadamu na mifugo”



Aidha  Mhe. Papian Amewapongeza wakazi wa Ngabolo kwa jitihada zao za kudumisha amani katika kijiji chao. Vilevile amekemea suala la uchungiaji mifugo kwenye mashamba ambapo amesema kwamba suala hilo linawatia umaskini wakulima ,hivyo wanaofanya vitendo hivyo waache mara moja ili kutokusababisha uvunjifu wa amani .


Mhe. Papian ametembelea kijiji cha Ngabolo,ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku saba katika vijiji mbalimbali vya jimbo lake kukagua shughuli za maendeleo sambamba na kuzungumza na wakazi wa vijiji husika. Akiwa katika kijiji cha Ngabolo Mhe. Papian  amekagua ujenzi wa madarasa kwa ajili ya uanzishaji shule ya Msingi katika kijiji hicho ambacho kwa sasa watoto wanalazimika kwenda shule katika kijiji cha Ndedo ambacho kiko umbali mrefu kutoka kijijiNgabolo. Pia amekagua bwawa ambalo la kijiji hicho ambalo limepasuka baada ya mvua nyingi zilizonyesha mwaka huu .



.............MWISHO...........

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUA: HATIMAYE KALOLENI YAPATA SHULE MPYA YA MSINGI

    July 30, 2025
  • SHULE YA MSINGI KINANGALI NAYO YANUFAIKA NA MRADI WA BOOST

    July 30, 2025
  • SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAENDELEA KUWEKEZA KWA VITENDO: KURASH YAPATA MRADI MWINGINE WA MILIONI 153 KUPITIA BOOST

    July 30, 2025
  • KATA YA BWAWANI YAPATA MRADI WA SHULE MPYA YA ELIMU MSINGI.

    July 28, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa