• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Azungumza na Watumishi wa Umma Wilayani Kiteto Leo Tarehe 05.07.2017

Imetumwa : July 5th, 2017

Mh. mkuu wa mkoa wa Manyara Dkt. Joel N. Bendera akizungumza na watumishi wa umma katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto.

Katibu tawala wa mkoa wa Manyara  Bw. E. Maswi akizungumza na watumishi  wa umma katika ukumbi wa halmashauri ya  wilaya ya  Kiteto

                   Mkuu wa wilaya  ya Kiteto Mh. T. Magessa akizungumza na watumishi  wa umma katika  mkutano huo.

Watumishi wa umma wakiwasikiliza kwa makini  viongozi wao kama inavyoonekana katika picha.


Habari kamili.

Mh. mkuu wa mkoa wa Manyara Dkt. Joel N. Bendera amefanya ziara wilayani Kiteto kwa lengo la kuzungumza na watumishi wa umma. Katika ziara hiyo Mh. mkuu wa mkoa alifuatana na katibu tawala wa mkoa wa Manyara  Bw. Eliakimu Maswi pamoja na maafisa waandamizi kutoka katika ofisi ya mkuu wa mkoa  wa  Manyara.


 Akizungumza na watumishi wa umma katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Mh. mkuu wa mkoa wa Manyara amesema  kwamba kila mtumishi  wa umma anatakiwa kuwajibika ipasavyo katika kutekeleza majukumu yake. Uwajibikaji huo lazima uende sambamba na kufanya kazi kwa pamoja (team work) ambapo  watumishi wote pamoja na wakuu wa idara wanatakiwa kufanya kazi kwa pamoja .Aidha mkuu wa mkoa  amewataka wakuu wa idara kuwa na maono, uthubutu na uzalendo katika utekelezaji wa majukumu yao, moyo wa uzalendo ni muhimu ili kuweza kusimamia kwa uangalifu,rasilimali zilizopo pamoja na mapato,na kuwa  wabunifu na wenye bidii katika kutekeleza majukumu yao   ili kutomkwamisha mkurugenzi wa halmashauri. Mkuu wa mkoa pia amewataka watumishi wa  umma kubadili mitazamo yao, ili kuweza kuenda sambamba na kasi  ya awamu ya tano.


Katika mkutano huo, katibu tawala wa mkoa wa Manyara amesisitiza uadilifu, ambapo watumishi wote wa umma wametakiwa kuwa waadilifu katika utumishi wao, kwani uadilifu ndio utakaowawezesha  kuwatumikia vema wananchi kwa kuwapa  huduma ambazo wananchi wataridhika na kwamba kwa kuwa waadilifu ndipo wataweza kujenga utumishi mzuri, usio na lawama kutoka  kwa wananchi.


Naye mkuu wa wilaya  ya Kiteto  mheshimiwa T
umaini Magessa amesema  kwamba  kila mtumishi abadilike ili kwenda  na kasi ya awamu ya tano, kama kauli mbiu ilivyo ya hapa kazi tu, ni kufanya kazi kweli kweli.Lazima watumishi wote wa umma wakubali  mabadiliko.


Pia mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto bwana Tamim Kambona amesema  kwamba uwezo wa halmashauri kimapato bado ni mdogo ukilinganisha na huduma ambazo halmashauri inatakiwa kuzitoa kwa wananchi na ukubwa wa eneo la wilaya ya Kiteto kijografia lakini watumishi wote wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano, kuacha kuongea mambo ambayo hayana tija, na badala yake waongee yale ambayo yatasaidia kuwajenga zaidi ili kuboresha utendaji kazi katika halmashauri. Kadhalika Mkurugenzi  amewataka  wakuu wa idara kufanya kazi kwa bidii, na pale wanapokutana na changamoto yoyote wamshirikishe ili kwa kushirikiana nae waweze kutatua changamoto hizo.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa